Kocha
Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez, ameibuka na kusema kuwa, timu ya
Yanga ambayo wamepangwa nayo kundi moja kwenye michuano ya Kombe la
Mapinduzi, ndiyo itakuwa kipimo chao kikubwa kama wapo fiti.
Katika
michuano hiyo inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 30, mwaka huu
visiwani Zanzibar, Azam na Yanga zimepangwa Kundi B sambamba na Zimamoto
na Jamhuri.
Ofisa
Habari wa Azam FC, Jaffar Idd, amesema: “Kocha wetu Zeben tayari
amekiandaa vizuri kikosi chake na amebaini kwamba kundi letu ni gumu
kutokana na timu zilizopo ikiwemo Yanga.
“Kama
tujuavyo, Yanga inapokutana na Azam kunakuwa na ushindani wa hali ya
juu, hivyo amesema ni kipimo sahihi kwa wachezaji wake kuonyesha umahiri
wao, ikiwezekana kuwa mabingwa kabisa.”
Aidha
Idd alisema kikosi chao kinatarajiwa kwenda visiwani humo Ijumaa au
Jumamosi baada ya kumaliza mechi yao ya ligi kuu dhidi ya Prisons
itakayopigwa Alhamisi usiku kwenye Uwanja wa Azam Complex jijini Dar.
SOURCE: CHAMPIONI
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment