Kesi
ya uchochezi dhidi ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jana
imeendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam
ambapo upande wa Mashtaka umetoa ushahidi wa pili.
Lissu
anakabiliwa na mashtaka ya kutoa kauli za kichochezi na maudhi dhidi ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.
Shahidi
huyo wa pili aliyetambulishwa kama ASP Kimweri, alisema kauli ya Lissu
aliyoitoa June 28 mwaka huu kuhusu ‘Dikteta uchwara’, ililenga katika
kufanya uchochezi na ilikuwa ya maudhi dhidi ya Rais na ililenga
kuchochea wananchi kuipinga na kuichukia Serikali.
Akizungumza
mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwampamba, shahidi huyo aliongeza kuwa
kauli hiyo ya Lissu pia ililenga katika kuhatarisha usalama wa taifa
kama ingesambazwa sehemu kubwa.
Naye
Wakili wa Lissu, Peter Kibatala alimtaka shahidi huyo kuieleza mahakama
ni nani ambaye mteja wake alikuwa anamtaja kama ‘dikteta uchwara’ na
taifa analolizungumzia kwenye madai yake.
Akijibu
maswali ya Wakili Kibatala, ASP Kimweli alisema kuwa hakufahamu
kiuhalisia ni nani ambaye Mbunge huyo alikuwa akimrejea katika matamko
yake na pia hakufahamu ni taifa gani alilokuwa akilimaanisha.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 18 mwakani itakaposikilizwa tena mahakamani hapo. Lissu yuko nje kwa dhamana.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment