Serikali
inafanya uchunguzi kuhusu tuhuma zilizoripotiwa na vyombo vya habari
vya Malawi kuwa vimewakamata ‘mashushu’ nane wa Tanzania wakijaribu
kuingia kinyamela kwenye mgodi wa ‘uranium’.
Taarifa
zilizoripotiwa na vyombo vya habari nchini humo juzi zimedai kuwa watu
hao nane walikuwa wapelelezi na kwamba walitaka kuingia kwenye mgodi huo
kujaribu kuchunguza kama nchi hiyo inatengeneza ‘nyuklia’ katika eneo
la Kayerekera. Ripoti iliyowekwa kwenye mitandao mbalimbali ya Malawi
pia imedai kuwa watu hao waliingia nchini humo bila kuwa na nyaraka za
kusafiria.
Akizungumzia
madai hayo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
Dk. Augustine Mahiga jana alifanya mahojiano na The Citizen na kueleza
kuwa hakuwa na taarifa hizo lakini atazifuatilia kwa kina na kufanya
uchunguzi kwani ni tuhuma kubwa na nyeti.
“Ndio
ninasikia hilo kwa mara ya kwanza kutoka kwako. Hizi ni tuhuma kubwa,
nitafuatilia kwa kina leo (jana) jioni kwa kuwasiliana na ubalozi wetu
wa Malawi kufahamu kama wanafahamu lolote kuhusu hili,” Dk. Mahiga
anakaririwa.
Hata
hivyo, tofauti na ripoti zilizotolewa kwenye vyombo vya habari vya
Malawi, Msemaji Msaidizi wa Polisi wa eneo la Karonga, George Mlewa
alikana ripoti hizo akidai kuwa watu hao nane waliokamatwa wanachukuliwa
kama wahamiaji haramu tu.
“Wakati tunaendelea na uchunguzi wetu kuhusu suala hili, naweza kusema kuwa ripoti hizo ni uvumi tu,” alisema Mlewa.
Chanzo: The Citizen
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment