Wakazi wa mtaa wa Keko Machungwa kata ya Miburani wilaya Temeke jijini
Dar es salaam wamedai mtaa wao unakabiliwa na changamoto ya ongezeko
kubwa la watoto wanaoingia kwenye ushoga hali ambayo ina hatarisha
malezi ya watoto wengine ambao wanaishi katika mtaa huo.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Keko Machungwa Mr Mashaka (katikati)
Hayo yameibuliwa na Mwenyekiti wa Mtaa wa Keko Machungwa Mr Mashaka
Ramadhani baada ya kutembelewa katika mtaa wake na wanafunzi ambao
wanapambania haki za watoto kutoka chuo kikuu cha Dar Es Salaam
University College of Education (DUCE) kwa ajili ya kutoa elimu ya haki
za watoto kwa baadhi ya watoto wa mtaa huo pamoja na wazazi ndipo
changamoto hiyo ikaibuka.
Akiongea mbele ya waandishi waliojitokeza katika mafunzo hayo,
Mwenyekiti huyo alidai mtoto wengi wanajiingiza katika matendo mabaya
kutokana na malezi mabaya ya mawazi pamoja na mtaa huo kujengwa
kiholela.
“Katika mtaa wetu kumekuwa na changamoto nyingi lakini kwa upande
wa watoto kumekuwa na wimbi la watoto kuingia kwenye ushoga kama
ulivyosikia,” alisema Mashaka. “Kwa hiyo ujio wa watu kama hawa katika
mtaa wetu unaweza kusaidia kutoa elimu kwa wazazi juu ya malezi bora,
kufuatilia mwenendo ya watoto wetu wakiwa shuleni na nyumbani pamoja na
kuangalia marafiki ambao anatembea nao,”
Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar Es Salaam University
College of Education (DUCE) Emijidius Cornel ambaye ni mmoja kati ya
wanafunzi walioandaa tukio hilo(kushoto) akiwa na Diwani wa kata hiyo,
Juma R. Mkenga
Pia mwenyekiti huyo alidai mtaa huo mwenye wakazi 12,400
unakabiliwa na ujenzi holela kutokana na viwanja na eneo hilo kutopimwa
hali ambayo imesababisha mtaa huo kuwa navichochoro vingi.
“Kuna changamoto nyingi kama nilivyosema lakini pia huu mtaa
viwanja vyake havijapimwa, kwa hiyo kumekuwa na mbanano wa nyumba sana
na wakazi ni wengi,”
Kwa upande wa Diwani wa kata ya hiyo Juma R. Mkenga ambaye pia
alikuwa mwenyekiti wa mtaa huo kabla ya kuwa Diwani, alikiri kuwepo kwa
watoto wa namna hiyo ambapo pia aliwataka wazazi wa mtaa huo kuwa makini
na watoto wao ili kuwaepusha kuingia kwenye janga hilo.
Mmoja kati ya wakazi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la
Mama Happy, alidai watoto wao wapo kwenye mazingira hatarishi kutokana
na watoto wengi wa mtaa huo kuingia kwenye janga hilo.
“Hapa watoto ambao ni mashoga wapo wengi sana, yaani wapo wengi
mpaka wengine tunawajua kwa majina kabisa na idadi ni kubwa, tena
wengine hawajifichi kabisa, wanaeleza,” alisema mama huyo.
Mama huyo mwenye watoto wawili alidai watoto wa shule za msingi
wenye umri kuanzia miaka 10 na kuendelea ndio waathirika wakuu wa janga
hilo huku akiitaka serikali pamoja na wazazi kulifuatilia suala hilo kwa
ukaribu zaidi.
“Suala hili kwa upande wangu naona lina sababishwa na wazazi
kutowafuatilia watoto wao, mzazi mtoto toka anaanza la kwanza hadi la
saba hajawahi kwenda shule wala kujua mtoto wake anafanya nini shule.
Kwa hiyo watoto wengi wanadanganya wapo shule kumbe wapo vichakani
wanafanya vitu vyao,” alisema Mama huyo.
Aliongeza “Pia yaha mambo yamesababishwa na vikundi, wengine tamaa
za maisha kutoka mashuleni, uvutaji wa bangi pamoja na uhuru mwingi
wanaopewa na wazazi. Mimi na mtoto mmoja wa kike na mwingine wakiume
lakini ukifika muda wa jioni tu nahakikisha mtoto wangu wapo ndani kwa
sababu hii hali sio nzuri na inatisha, nimekaa sehemu nyingi lakini mtaa
huu kiboko,”
Mzazi huyo ameiomba serikali ya mtaa pamoja na serikali ya mkoa wa
Dar es salaam kufuatilia sakata hilo kwa makini ili kujaribu kulidhiti
haraka iwezekanavyo.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment