Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema amekuwa kimya muda mrefu kuhusiana na kupotea katika mazingira ya kutatanisha, msaidizi wake Ben Saanane kwa kuwa suala hilo lipo kwenye uchunguzi.
Mbowe alisema hayo
jana alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Mbeya wakati
wa uchaguzi wa viongozi wa chama hicho Kanda ya Nyasa inayojumuisha
mikoa ya Iringa, Mbeya, Songwe, Njombe na Rukwa.
Alisema yeye pia
ameathiriwa na tukio hilo kama ilivyo kwa wazazi wake na ndugu wengine
kwa kuwa ni mtu muhimu kwake katika kutekeleza majukumu yake.
“Ndugu
zangu Watanzania msione nipo kimya, nimefanya hivi kutokana na kuwa
suala hili lipo kwenye uchunguzi kwani tukizidisha kuongea ongea wale
ambao wamemteka wanaweza kupoteza uhai wake kisa maneno,” alisema Mbowe.
Alisema, “Chadema ni taasisi ambayo ina vyombo vya ulinzi na usalama
ambavyo vinaendelea kuchunguza tukio hili la aina yake.”
Katika hatua
nyingine, Mbowe aliishitumu Serikali akidai kwamba imeendelea kuwafunga
wanachama wake na kwamba mpaka sasa 180 wapo mahabusu. Alisema hizo ni
jitihada za kuua nguvu za upinzani.
Akijibu madai hayo, Kamishna wa
Polisi (Operesheni na Mafunzo), Nsato Marijani alisema jeshi hilo
linawashikilia watu wengi kwa makosa mbalimbali vituoni na wengine
mahabusu katika
magereza. Alisema polisi haimkamati mfuasi wa chama cha siasa bali mtu
anayekwenda kinyume cha sheria.
“Hayo yanayosemwa siyo ya kweli, waache
kulipaka tope jeshi la polisi. Tutaendelea kuwakamata watu wote
wanaovunja sheria. Hata kama akiwa mjomba wangu tutamkamata.”
Msigwa
kidedea
Katika uchaguzi huo, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliibuka kidedea baada ya kushinda kwa kupata kura za
ndiyo 62 sawa na asilimia 58.49 kati ya kura 106 zilizopigwa.
Akitangaza
matokeo hayo, msimamizi wa uchaguzi huo Naibu Katibu Mkuu wa Chadema
(Bara), John Mnyika alisema nafasi ya makamu mwenyekiti imechukuliwa na
Sadrick Malila ambaye alipata kura za ndiyo 93 sawa na asilimia 88 ya
kura zilizopigwa 106 huku kura tatu zikiharibika.
Mnyika alisema kuwa nafasi ya mweka hazina imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, Sophia Mwakagenda ambaye alishinda kwa kupata kura 91 ambayo ni sawa na asilimia 86 kura zote 106 zilizopigwa.
Mnyika alisema kuwa nafasi ya mweka hazina imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, Sophia Mwakagenda ambaye alishinda kwa kupata kura 91 ambayo ni sawa na asilimia 86 kura zote 106 zilizopigwa.
Mnyika alisema katika uchaguzi huo wajumbe walipiga kura za ndiyo au
hapana kwa lengo la kufanya uchaguzi wa maridhiano kwani uchaguzi wa
kuweka wagombea wawili husababisha makundi na kuleta migogoro ndani ya
chama.
“Hivyo Kamati Kuu Taifa baada ya kuliona hilo tukaamua kuwaita
wagombea wote na kuwaeleza nia yetu ya kufanya hivyo na hatujafanya huku
tu, hata kanda nyingine tulizopita tumefanya hivyo" Alisema Mnyika
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment