Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru washitakiwa wanne kati ya 10
waliokuwa wanakabiliwa na mashitaka ya mauaji ya bila kukusudia ya
aliyekuwa Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Dk Sengondo Mvungi.
Washitakiwa
walioachiwa ni Masunga Makenza (40), mkazi wa Tabata Darajani, Zacharia
Msese (33), Ahmad Kitabu (30) mkazi wa Mwananyamala na John Mayunga
(56).
Waliachiwa
kwa mujibu wa Kifungu Namba 91 Kifungu kidogo cha kwanza cha Mwenendo
wa Makosa ya Jinai (CPA). Wakili wa Serikali, Pamela Shinyambala alidai
mbele ya Hakimu Mkazi Thomas Simba kuwa upande wa mashitaka umeshasajili
jalada hilo Mahakama Kuu.
Hata
hivyo, Mkurugenzi wa Mshitaka Nchini (DPP), hakuwa na nia ya kuendelea
kuwashitaki washitakiwa hao kwa mujibu wa kifungu hicho. Awali,
Shinyambala alidai kuwa kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutolewa maelezo
ya mashahidi baada ya upelelezi wa kesi hiyo kukamilika.
Hakimu
Simba alisema anawaachia washitakiwa hao, kama walivyoomba upande wa
mashitaka. Alisema kwamba washitakiwa sita, ndio watakaosomewa maelezo
hayo ya mashahidi.
Washitakiwa
hao ni Longishu Losingo (29), Paulo Mdonondo (30) mkazi wa Tabata
Darajani, Mianda Mlewa (40) Mkazi wa Vingunguti, Juma Kangungu (29)
mkazi wa Vingunguti, Msungwa Matonya (30), mkazi wa Vingunguti na
Masenga Mateu.
Hata
hivyo, Hakimu Simba aliutaka upande wa mashitaka, kuhakikisha kwamba
wanaleta cheti cha kifo cha mshitakiwa wa kwanza, Chibago Magozi (32),
mfanyabiashara mkazi wa Vingunguti Machinjioni.
Pia
alieleza kuwa kesi hiyo ikienda mahakama kuu, bila ya kupelekwa
mahakamani hapo cheti cha kifo, itakwama kwa kuwa hawawezi kusoma
maelezo hayo hadi kwa mtu aliyekufa.
Aliwataka kuhakikisha katika tarehe ijayo ambapo washitakiwa sita watasomewa maelezo, wawe wamewasilisha cheti cha kifo.
Hata
hivyo, Wakili Shinyambala alikubaliana na maelezo hayo na kuomba tarehe
nyingine kwa ajili ya kuwasomea washitakiwa waliobaki maelezo ya
mashahidi. Kesi imepangwa Januari 10, 2017.
Download Application ya Hebron Male Blog Kwenye Simu yako Kusoma Habari Zetu Kwa Urahisi
0 comments:
Post a Comment