WAZIRI
wa Habari,Utamaduni,Wasanii na Michezo,Nape Nnauye amewatoa hofu
wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini hususani Magazeti pamoja na
wanahabari kwa kusema hatafungia magazeti badala yake atahakikisha
anakuwa mlezi wa vyombo vya habari pamoja waandishi wa habari ili viweze
kufanya kazi kwa weredi.
Akizungumza
na wafanyakazi wa wizara ya Habari na utamaduni,wasanii na Michezo
wakati alipokuwa akipokelewa na wafanyakazi wa wizara hiyo kwa mara ya
kwanza tangu achaguliwe kwenye nafasi hiyo na Rais Magufuli, Nape
amesema baada ya Rais Magufuli kumchagua kuwa Waziri wa wizara hiyo
waliibuka watu wakisema magazeti yatafungiwa.
“Nawaomba
watu wa sekta ya habari kuondoa dhana ya kwamba mimi nitakuwa mtu wa
kuyafungia magazeti.Kitu kama hicho hakipo kwani nimekuja kwenye wizara
hii ili wanahabri wafanye kazi kwa weredi .Ninawahahidi nitakuwa mlezi
wa vyombo vya habari”amesema Nnauye.
Amesema
anafahamu kwa sasa sheria ya magazeti ya mwaka 1976 imekuwa
ikilalamikiwa sana,hivyo ameahidi kulishughulikia suala hill.
.
Hata
hivyo Nape ambaye ni mbunge wa Jimbo la Mtama,amewaomba wanahabari
pamoja na wamiliki kuhakikisha wanafanya kazi kwa weredi ili kuhakikisha
wanaiweka jamii kwenye nafasi nzuri ya Amani kwa madai kuwa wanahabri
wananafasi kubwa katika jamii ya kuilinda amani.
Kwa
upande wake Naibu waziri wa wizara hiyo Anastazia Wambura amewataka
watendaji wote wa wizara hiyo kufanya kazi kwa ufanisi mkubwa ili waende
sawa na jinsi Rais Magufuli anavyoenda na kasi ya kuwatumikia
watanzania.
Lukuvi Akaribishwa Wizara ya Ardhi
Waziri
wa Ardhi nyumba na maendelea ya Makazi,William Lukuvi ambaye
amerejeshwa tena kwenye wizara hiyo baada ya uteuzi wa Rais
Magufuli,amewataka viongozi wa wizara hiyo ndani ya siku saba
wampelekee mipango mipya ya kiutendaji lasivyo mtendaji ambaye
atashindwa kumpelekea taarifa ya mipango hiyo atafukuzwa kazi.
Waziri
Lukuvi ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam wakati akikaribishwa
tena na wafanyakazi wa wizara hiyo mara baada ya kurejeshwa tena na Rais
Magufuli ambapo amesema kwa sasa anataka watumishi wote wafanye kazi
kwa kasi ya Rais Magufuli huku akiwataka mpaka jumatatu wapeleke taarifa
ya mipango kwa kila mtendaji wa wizara hiyo.
Amesema
nia ya kuhitaji taarifa ya mipango hiyo ni kutaka kufahamu maeneo yapi
muhimu kwa sasa kwa wananchi ili iwe rahisi kuwatumikia,
Sanjari na hilo Waziri Lukuvi ametoa kalipia kwa watu wote wanaomiliki mashamba ambayo wameshindwa kuyatekeleza kwa wakati na kusema kuwa wizara yake itahakikisha mashamba hayo wananyang’anywa na kurudishwa serikalini kwa ajili ya kupewa watu wengine wenye nia ya kuyatumia mashamba hayo.
Jaffo Naye Aibukia Bahi
Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Utumishi na Utawala Bora, Selemani Jaffo amewatangazia kiama wakurugenzi wote nchini watakaoshindwa kuwasimamia wakuu wa idara katika Halmashauri zao.
Naibu
huyo alitoa kauli hiyo jana alipofanya ziara yake ya kikazi ya kwanza
ya kushtukiza katika wilaya ya Bahi iliyopo mkoani Dodoma.
Mbali
na hilo ametoa muda wa siku 27 kwa halmashauri zote nchini kuhakikisha
zinatumia mfumo wa kielektroniki kwa ajili ya kukusanya mapato katika
halmashauri husika.
Jaffo
amesema kwamba mfumo wa kizamani wa ukusanyaji mapato unachangia kwa
kiasi kikubwa cha watumishi wengi pamoja na wakurugenzi kufanya ufisadi
na kupiga fedha ya Umma.
Katika
hatua nyingine amewaagiza watumishi wote katika halmashauri ya Bahi
pamoja na halmashauri nyingine nchini kuhakikisha hawakai maofisini na
badala yake watembelee miradi na kujua matatizo ya wananchi.
Amesema
hakuna haja ya watumishi kukaa maofisini kwa ajili ya kusubiri taarifa
ambazo wakati mwingine ni za upotoshaji na kusababisha wananchi
kuichukia serikali yao.
0 comments:
Post a Comment