MKUU
wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Mohamed Utaly amewaweka ndani
wafanyabiashara 21 kwa saa 6 kwa kukiuka agizo la Rais la kufanya usafi
na kufungua maduka kabla ya muda ulioelekezwa.
Mkuu
huyo wa wilaya alichukua hatua hiyo juzi, baada ya wafanyabiashara hao
kufungua maduka kabla ya saa nne Sikukuu ya Uhuru ya Desema 9, mwaka
huu, huku wananchi wakiendelea na usafi katika maeneo mbalimbali ya mji
wa Mpwapwa na viunga vyake.
Akizungumza
na wananchi hao mara baada ya kumaliza kufanya usafi katika viwanja vya
Mnara wa Mashujaa, mkuu huyo wa wilaya aliwataka wananchi kuzingatia
maagizo yatolewayo na viongozi wa Serikali kwa lengo la kuongeza
ushirikiano zaidi.
Pia
aliwataka kuendeleza utamaduni wa usafi kila baada ya wiki mbili na
kuongeza kuwa watatunga sheria ndogo ya utunzaji wa mazingira katika mji
wa Mpwapwa na viunga vyake.
Hata
hivyo, wananchi walilalamikia halmashauri ya Mpwapwa kwa kushindwa
kuweka vituo vya kukusanya taka na kusababisha wananchi kuvamia maeneo
ya wazi na kutupa taka hovyo.
Alisema
kukosekana kwa gari la usombaji taka katika mji wa Mpwapwa, ndio chanzo
kikuu cha mji huo kuendelea kuwa mchafu. Mkurugenzi Mtendaji wa
halmashauri hiyo, Mohamed Maje alikiri kuwepo kwa changamoto hiyo ya
kukosa gari la kusomba taka.
Kuhusu
vituo vya kukusanyia taka, aliamuru Ofisa Usafi na Mazingira wa
halmashauri hiyo, Emanuel Sallo kukaa na wadau ili kuainisha maeneo
hayo.
0 comments:
Post a Comment