Rais
wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtumia
salamu za pongezi mbunge wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye kufutia
kuteuliwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo katika
serikali ya awamu ya tano.
Katika
salamu zake, Malinzi amempongeza Nape na kusema TFF ina imani nae
katika nafasi hiyo, na kuahidi kushirikiana katika michezo na haswa
katika kusukuma gurudumu la maendeleo ya mpira wa miguu nchini.
Aidha
pia Malinzi amewapongeza Paschal Kihanga, Mwenyekiti wa chama cha soka
moa Morogoro kwa kuchaguliwa kuwa Meya wa manispaa hiyo, na James Bwire
mmiliki wa shule ya Alliance kwa kuchaguliwa meya wa manispaa ya
Nyamgana.
Malinzi
amewatakia kila la kheri katika nafasi hizo walizozipata za kuwatumikia
watanzania, na kwa niaba ya familia ya mpira wa miguu nchini anawatakia
kila la kheri na kuahidi kushirikiana nao.
0 comments:
Post a Comment