Baada
ya kusambaa kwa taarifa kwenye mitandao zikieleza kuwa kampuni ya Home
Shopping Centre imefunga maduka yake kutokana na kukwepa kodi na
kuhusika kwenye sakata la makontena yaliyopotea bandarini, uongozi wa
kampuni hiyo umejitokeza na kupinga taarifa hizo.
Kupitia
taarifa yake kwa vyombo vya habari, kampuni hiyo imeeleza kuwa habari
hizo sio za kweli na kueleza kuwa haijawahi kukwepa kodi na haihusiki
kwa namna yoyote na makontena yaliyopotea bandarini.
“Home
Shopping Centre Co. Limited haihusiki kabisa kwa njia yoyote ile na
wizi, ukwepaji kodi, au potevu wa makontena 349 na yale zaidi ya 2431
yaliyoibuliwa na Mheshimiwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kamwe
haijawahi kujihusisha na uhalifu huo wa kuiba makontena na kukwepa
kodi,” ilieleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mfilisi wa kampuni hiyo,
Yusufu Mohamed.
Mohamed alieleza kuwa kampuni hiyo ilifunga maduka yake kama ambavyo makampuni mengine hufanya na sio vinginevyo.
0 comments:
Post a Comment