UFAFANUZI WA MASUALA MBALI KWA WATEJA WA TANESCO KUPITIA VYOMBO VYA HABARI.
1. HALI YA UZALISHAJI UMEME NCHINI
Hali ya umeme nchini imeendelea kuimarika licha ya changamoto mbali mbali tunazokabiliana nazo kwa sasa. Kuanzia taerehe 17 Septemba tulipoanza kutumia gesi inayotoka Mtwara tumeweza kuongeza uzalishaji wa umeme unaotumia gesi kutoka Megawati 260 zilizokuwepo kabla hadi Megawati 560 ikiwa ni ongezeko la jumla ya Megawati 300 au asilimia 115 ya umeme wa gesi uliokuwa unazalishwa. Hii imechangia sana kuboresha hali ya umeme tofauti na ilivyokuwa hapo kabla.

Tunategemea
kuongeza umeme wa Megawati 130 zaidi kutokana na vyanzo vya Gesi kati
ya sasa na mwishoni mwa mwezi Januari 2016. Hii itafanya jumla ya umeme
wote unaotokana na gesi kufikia Megawati 700 sawa na asilimia 70 ya
umeme wote kwenye Gridi ya Taifa.
Haya
ni mapinduzi makubwa kwani kwa miaka mingi vyanzo vya maji ndivyo
vimekuwa vikichangia zaidi ya asilimia 70 ya umeme nchini na hivyo
kusababisha athari za mara kwa mara kila unapotokea ukame.
Pamoja
na hayo yaliyokwishafanyika, Mkandarasi wa mradi wa pili wa Kinyerezi
(KII) wa Megawati 240 anatarajia kuanza kazi wakati wo wote kuanzia sasa
baada ya kuwa amekwishalipwa sehemu ya fedha za awali za kuanza kazi
hiyo.
2. MIUNDOMBINU YA TANESCO
Miongoni mwa kero kubwa inayolalamikiwa sana na wateja wetu ni kukatika umeme kunakosababishwa na uchakavu wa miundombinu. Ukweli ni kwamba baadhi ya miundombinu tuliyo nayo ni ya siku nyingi wakati matumizi ya umeme
yameendelea kuongezeka kwa kasi sana.

Kwa
mfano nyingi ya Substations katika jiji la Dar es Salaam zimejengwa
katika miaka ya 80 na 90. Wakati huo wakazi wa jiji la Dar es Salaam
walikuwa chini ya milioni 3. Sasa hivi wakazi wa jiji ni zaidi ya
milioni 5 na hivyo miundombinu iliyopo inaelemewa sana.
Jitihada
za kurekebisha hali hii zilikwishaanza ambapo sasa kuna miradi mikubwa
inaendelea katika jiji la Dar es Salaam na itakapokamilika itasaidia
sana kupunguza tatizo la kukatika kwa umeme. Kwa kiasi fulani kukatika
huko kwa umeme hasa katika jiji la Dar es Salaam kunatokana pia na
utekelezaji wa miradi hiyo.
Miradi
inayotekelezwa ni pamoja na ule unaojengwa kusini mwa Dar es Salaam kwa
mkopo wa Benki ya Dunia ambao utaboresha umeme maeneo ya Kigamboni,
Kurasini, Mbagala, Mkuranga, Kisarawe, Gongolamboto, Ukonga, Kitunda,
Vingunguti na Tabata
Mradi
mwingine ni unaotekelezwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan ambao
utasaidia kuondoa matatizo yaliyo katika maeneo ya Muhimbili na Upanga,
Mwananyamala na Kinondoni, Oysterbay na Masaki, Jangwani Beach, Bahari
Beach na Mbezi Beach.
Mradi
mwingine ni ule unaotekelezwa kwa mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya
Afrika ambao unaendelea katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha,
Shinyanga, na Geita.
Mradi
mwingine ni ule unaofadhiliwa na Serikali ya Finland ambao utasaidia
sana kuimarisha umeme kati kati ya jiji la Dar es Salaam na kusaidia
kuimarisha umeme katika eneo lenye majengo mengi marefu la Samora,
Azikiwe, Kariakoo na Sea view.
Sambamba
na miradi hiyo inayotekelezwa Dar es Salaam, mradi mkubwa wa kupeleka
umeme wa 400KV kutoka Iringa kupitia Mtera, Dodoma, Singida hadi
Shinyanga uko kwenye hatua za mwisho za kukamilika na hivyo
kutuhakikishia umeme wa uhakika katika kanda ya ziwa hasa jiji la
Mwanza.
Kazi ya kuunga Songea na Gridi ya Taifa kutokea Makambako kwa 220KV inaendelea na Makandarasi wako kazini.
Kazi ya kuunga Songea na Gridi ya Taifa kutokea Makambako kwa 220KV inaendelea na Makandarasi wako kazini.
Kazi
za kuunga Tanzania na Kenya kwa umeme wa 400KV inatarajiwa kuanza hivi
karibuni kwani zabuni za kuwapata Makandarasi ziko katika hatua za
mwisho. Ujenzi unategemewa kuanza mwakani.
Kazi
nyingine ambazo hazijaanza lakini zitaanza hivi karibuni ni pamoja na
Dar es Salaam – Somanga (400KV), Bulyankhulu – Geita – Nyakanazi –
Rusumo (220KV)
Miradi
hii ya kuimarisha miundombinu ikikamilika itasaidia kulipunguza kwa
kiasi kikubwa tatizo la kukatika kwa umeme kutokana na mfumo wa
Usambazaji.
Nawaomba
wateja wetu, wakati kazi hii kubwa inapoendelea, wawe na subira na
uvumilivu kwa usumbufu wa hapa na pale utakaokuwa unatokea. Hata hivyo
TANESCO itajitahidi kurekebisha kasoro zinazoweza kurekebishwa katika
miundombinu ya sasa ili kupunguza usumbufu huo wakati marekebisho
makubwa yakiendelea.
3. KERO ZA HUDUMA KWA WATEJA
Ukiacha kero zinazosababishwa na Miundombinu, TANESCO inachukua hatua madhubuti za kuwaadibisha wafanyakazi
wake wanaotoa huduma mbaya na kuwa kero kwa wateja. Baadhi ya kero ambazo zimekuwa zikilalamikiwa ni pamoja na lugha mbaya, wateja kudaiwa rushwa kabla ya kupewa huduma, kucheleweshewa huduma, ubadhirifu nk.

Shirika
linapenda kuwahakikishia wateja wake kuwa tayari limeshaanza kuchukua
hatua kali kwa wafanyakazi wanaobainika kujihusisha na mambo hayo. Kwa
mfano katika kipindi cha miezi miwili Shirika limewaachisha kazi maofisa
7 waandamizi kutokana na makosa mbali mbali ikiwemo wizi na
ubadhirifu.
Miongoni
mwao ni wale waliofikishwa mahakamani kule Kagera na kuripotiwa na
vyombo vya habari jana. Walioachishwa kazi ni pamoja na wafanyakazi wa
ngazi za Mameneja, Wahandisi na Wahasibu.
Shirika
litaimarisha hatua hizo ambapo mfanyakazi ye yote atakayebainika
analaghai wateja, anadai rushwa, anatoa lugha chafu au huduma mbovu
atawajibishwa mara moja na pale atakabobainika kuachishwa kazi.
Tumeanza
maandalizi ya kutoa namba maalum za simu kwa wateja wetu ambazo
zitatumika kutoa taarifa ya vitendo kama hivyo vinavyofanywa na
wafanyakazi wetu ili hatua muafaka ziweze kuchukuliwa dhidi yao.
4. KUDHIBITI WIZI WA UMEME
Shirika linaendelea na Kampeni maalum katika mikoa yote ya kuwakamata wezi wa umeme na kuwachukulia hatua kali. Pamoja na hatua nyingine zitakazochukuliwa, wezi wa umeme watakuwa wanatangazwa hadharani na kufunguliwa mashtaka.

Hivyo
ninatoa rai kwa ye yote ambaye amekuwa akijihususha na wizi wa umeme
ajisalimishe mwenyewe kwa kwenda kwa Meneja wa Mkoa anakopatia huduma.
Kama
hawatajisalimisha kwa hiari hatua zilizokusudiwa dhidi yao zitachukuliwa pasipo huruma yo yote.
hawatajisalimisha kwa hiari hatua zilizokusudiwa dhidi yao zitachukuliwa pasipo huruma yo yote.
Tunatoa
siku saba kwa wateja wanaojua kwamba mita zao zimechezewa kujisalimisha
wao wenyewe la sivyo TANESCO haitalaumiwa kwa hatua tutakazochukua.
5. UNUNUZI WA NGUZO KUTOKA KWA WAZALISHAJI WA NDANI
Tunapenda kufafanua kwamba Wazalishaji nguzo wa ndani ya nchi wana nafasi sawa ya kuuza nguzo zao TANESCO kwa mujibu wa sheria ya manunuzi.
Tunapenda kufafanua kwamba Wazalishaji nguzo wa ndani ya nchi wana nafasi sawa ya kuuza nguzo zao TANESCO kwa mujibu wa sheria ya manunuzi.
Hivi
karibuni baadhi ya vyombo vya habari vilidai kwamba TANESCO inakusudia
kununua nguzo 700,000 kutoka Afrika Kusini kwa dola za Marekani 115
milioni! Taarifa hizo ni za uongo na uzushi wa hali ya juu.
Kwa
mfano; TANESCO itawezaje kununua nguzo kwa dola miliomi 115! Hizo ni
fedha nyingi mno ambazo huenda zingetosha kuwekeza Mtambo mpya wa umeme
wa zaidi ya Megawati 100. Itazipata wapi fedha hizo kwa ajili ya kununua
nguzo tu?
Ukweli
ni kwamba tuna wasambazaji kadhaa wa nguzo kutoka ndani ya nchi na
wengine kutoka nje. Wote hupatikana kwa ushindani kulingana na Sheria ya
Manunuzi. Vigezo vinavyozingatiwa ni Ubora wa nguzo zao na bei.
Baadhi
yao waliwahi kupata zabuni lakini wakashindwa kuleta nguzo ikabiidi
zabuni ile ivunjwe na Waziri, baadhi yao ililazimu kuwanyang’anya zabuni
na kuwapa wa nje baada ya kushindwa kusambaza nguzo na kusababisha
malalamiko mengi kutoka kwa wateja.
6. USHIRIKI WA TANESCO KWENYE ZOEZI LA USAFI TAREHE 9 DESEMBA 2015
Wafanyakazi wote wa TANESCO watashiriki katika shughuli mbali mbali za usafi wa mazingira katika maeneo yote yanayozunguka ofisi, mitambo na vituo vyetu nchi nzima. Hii inaenda sambamba na agizo la Mh. Rais la kuitumia siku ya tarehe 9 Desemba kwa ajili ya shughuli za usafi.

Hii
itahusisha pia usafi kwenye substations, kando kando ya Transforma na
maaeneo mengine yenye miundombinu yetu. Tayari maandalizi ya kazi hizo
yamekwishaanza na tutashiriki kikamilifu.
Ahsanteni kwa kunisikiliza
0 comments:
Post a Comment