Waziri mkuu wa awamu ya tatu Mh.Fredirick Sumaye amtangaza rasmi
kujiunga na chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema na amekabidhiwa
kadi na Mwenyekiti wa chama hicho Mh.Freeman Mbowe.
Sumaye ambaye wakati wa uchaguzi alitangaza kujiondoa CCM na
kudai kuwa anaunga mkono mageuzi yanayofanywa na vyama vinavyounda
katiba ya wananchi (UKAWA) bila kuweka wazi kuwa yuko kwenye chama
kipi kati ya hivyo amesema asa ameamua kujiunga na CHADEMA.
Akizungumza katika mkutano wa kufunga kampeni za ubunge wa jimbo
la Arusha kwa chama cha CHADEMA uliofanyika kata ya baraa Sumaye
amesema anataka kuungana na wanamageuzi wenzake katika kuendeleza
harakati za mabadiliko hapa nchini ambazo bado zinaendelea.
Akizungumza baada ya kumkabidhi kadi Mwenyekiti wa chama hicho
Mh.Freeman Mbowe amesema chadema na vyama washirika wa UKAWA bado viko
imara na vimeendelea kuimarika na kwamba licha ya kudhulumiwa ushindi
azma yaoya kuleta ukombozi nchini iko pale pale.
Awali aliyekluwa mgombea uras wa CHADEMA akiwakilisha vyama vya
umoja wa katiba ya wananchi ukawa Mh.Edward Lowassa ameendelea kuwataka
watanzania wanaounga mkono mabadiliko kuwa watulivu na kwamba kwa vile
wana dhamira ya dhati ya kuyaona mabadiliko hakuna kukata tamaa kwani
bado kuna fursa yakufikiwa kwa malengo yao .
Chanzo
http://www.itv.co.tz/news
Chanzo
http://www.itv.co.tz/news
0 comments:
Post a Comment