Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (aliyevaa tai) akiwasalimia
wananchi wanaosubiri kupata huduma ya Hati za Kusafiria katika Ofisi
za Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar es Salaam
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga ameagiza waajiri kote
nchini kutowapa ajira wageni kwa kazi zinazoweza kufanywa na Watanzania.
Pia,
ameagiza maofisa wa Idara ya Uhamiaji kufanya operesheni maalumu
kuwatimua raia wote wasio na vibali vya kuishi nchini ifikapo Januari
31, 2016.
Kitwanga
ambaye alitembelea idara hiyo jana, alisema wizara yake kwa
kushirikiana na Uhamiaji imeanzisha operesheni ya kuwakamata raia wote
wa kigeni wanaoishi nchini kinyume cha sheria na kuwachukulia hatua
stahiki.
Waziri
huyo alisema kutokana na watu wengi kuishi nchini bila vibali, amewapa
mwezi mmoja Idara ya Uhamiaji kufanya uchunguzi katika maeneo yote ya
kazi na makazi, ili kuwaondoa walioingia nchini kinyemela.
“Katika
operesheni hii, tutahakikisha tunawakamata wote na nimetoa maelekezo
kwamba nitakuwa nikipewa ripoti kila Ijumaa kuanzia wiki ijayo, mpaka
ifikapo Januari 31 tuwe tumesafisha nchi kabisa,” alisema Kitwanga.
Alisema
kutokana na mpaka wa nchi kuwa mkubwa, Uhamiaji watawezeshwa ili
kukabiliana na tatizo la upitishwaji wa wahamiaji haramu kutoka nchi
mbalimbali, kama ilivyoripotiwa hivi karibuni.
Pia,
alitoa agizo kwa wananchi wa kawaida kuhakikisha wanatoa taarifa kuhusu
wahamiaji haramu walioweka makazi katika maghala, kampuni na viwanda
bubu ili kumaliza tatizo la wahamiaji haramu nchini.
Wafanyakazi wageni
Mbali
na maagizo hayo, Kitwanga pia aliagiza wamiliki wa kampuni mbalimbali
kuhakikisha hawatoi ajira kwa raia wa nje kwa kazi zinazoweza kufanywa
na Watanzania.
“…Lakini
kazi zote ambazo Watanzania wana utalaamu wa kuzifanya zitafanywa na
wazawa na si wageni na zile ambazo inaonyesha wazi kwamba Watanzania
hawana ujuzi huo, basi zifanywe na wageni,” alisema Kitwanga.
Kuhusu
vibali, Waziri Kitwanga alisema hakuna raia yeyote wa kigeni
atakayepata kibali cha kuishi nchini kama hajapata kibali cha kufanya
kazi kama amekuja kwa ajili ya kazi. Lakini utaratibu mwingine kama mtu
amekuja likizo utaendelea kama kawaida.
Kitwanga
alisema kuanzia Jumatatu ijayo, viongozi wa wizara husika na uhamiaji,
wakae wapange utaratibu mzuri utakaoonyesha kwamba hakuna usumbufu kwa
raia wa kigeni ambaye anakuja kufanya kazi nchini kwa kuzingatia vigezo.
Pasi za kusafiria
Aidha,
Waziri Kitwanga alisema mfumo wa uombaji wa pasi za kusafiria na vibali
vya ukazi, hivi sasa utakamilishwa kwa njia ya Tehama.
Alisema
mwombaji atatakiwa kufanyiwa mahojiano ya ana kwa ana pindi
atakapokamilisha utaratibu wa kujaza na kuzilipia fomu hizo benki, na
atapatiwa pasi ya kusafiria baada ya siku tatu huku kibali cha ukazi
akikipata baada ya siku tano ili kupunguza urasimu.
“Tumeafikiana uboreshaji wa namna ya kufanya kazi na kwa mtazamo wa mbali,” alisema.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akimsalimia
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile wakati alipowasili
Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini jijini Dar es Salaam jana kwa ajili ya
ziara ya kikazi. Wapili kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak
Abdulwakil, na kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo.
Kamishna
Jenerali wa Uhamiaji, Sylvester Ambokile (kushoto) akiwa na Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, wakati Waziri huyo alipokuwa
anafanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Uhamiaji, Kurasini, jijini Dar
es Salaam kwa lengo la kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanywa na
Uhamiaji. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (katikati) akiwaeleza jambo
Watendaji Wakuu wa Idara ya Uhamiaji wakati alipofanya ziara ya kikazi
Makao Makuu ya idara hiyo, Kurasini, jijini Dar es Salaam jana. Wapili
kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani
0 comments:
Post a Comment