Sunday, 27 March 2016

#YALIYOJIRI>>>>Magufuli, Museveni wampelekesha Uhuru.Fahamu zaidi hapa.

Kenya yafufua mazungumzo ya ujenzi wa bomba la mafuta na Uganda, lakini njia yake bado yaumiza vichwa
Dar es Salaam. Uamuzi wa Rais John Magufuli kukubali haraka mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta ghafi kutoka Hoima nchini Uganda hadi Tanga umemgutua Rais Uhuru Kenyatta, ambaye sasa anahaha kuishawishi Uganda ibadili msimamo wake.
Rais Yoweri Museveni na Magufuli walisaini makubaliano ya ujenzi wa bomba hilo la urefu wa kilomita 1,120 Machi Mosi, na kuifanya Uganda kuachana na mradi huo wa Dola 4 bilioni kupeleka bomba hilo hadi Lamu nchini Kenya.
Kenya na Uganda zilikubaliana katikati ya mwaka jana ujenzi wa bomba hilo, lakini hazikuafikiana njia ambayo lingepitia kutokana na sababu za kiusalama na hofu ya malipo ya fidia kwa wamiliki wa ardhi.
Uamuzi wa Rais Magufuli kukubali mradi huo utakaozalisha zaidi ya ajira 15,000 wakati wa ujenzi, ndiyo ulioharibu mipango ya Kenya, na sasa Kenyatta amefufua mazungumzo hayo.
Kenyatta alikuwa na mazungumzo na Museveni jijini Nairobi Jumatatu, lakini hawakuweza kufikia makubaliano na hivyo kupanga kukutana tena ndani ya wiki mbili jijini Kampala, linandika gazeti la Daily Nation la Kenya.
Katika taarifa iliyotolewa baada ya mazungumzo hayo, mawaziri wa nishati wa Uganda na Kenya walitangaza kuwa kikao hicho kilikuwa na mafanikio na kilijikita katika kupunguza gharama za ujenzi na sehemu ya kupitishia bomba hilo.
Mkutano ujao utawapa fursa mawaziri hao kuwasilisha mpango mmoja wa jinsi ambavyo bomba hilo litajengwa ikiwa ni pamoja na gharama za usafirishaji mafuta.
Daily Nation iliripoti mapema wiki hii kuwa utafiti uliofanywa na kampuni za mafuta ndiyo ilikuwa suala kubwa lililojadiliwa na marais hao wawili jijini Nairobi Jumatatu.
Gazeti hilo limemkariri ofisa mmoja kutoka Wizara ya Nishati akisema utafiti wa kampuni za Tullow Oil plc na China National Offshore Oil Company (CNOOC) umeionya Uganda dhidi ya kuendelea na mpango wake wa kujenga bomba hilo kutoka Hoima, kupitia Lokichar (kaskazini mwa Kenya) hadi Lamu.
“Inaeleweka kuwa kampuni hizo mbili zinazofanya kazi pamoja na Total ya Ufaransa zilionya kuwa mkakati wa Uganda kuanza kuchimba mafuta kwa ajili ya kuuza nje ifikapo mwaka 2018, unaweza kucheleweshwa kama itaendelea na njia ya Kenya,” linaandika gazeti la Daily Nation.
Katika kikao hicho, Rais Museveni aliwasilisha matokeo ya utafiti huo kuonyesha sababu za mpango wake wa hivi karibuni wa kuelekeza nguvu kwenye njia ya Tanzania.
Gazeti hilo limekariri vyanzo vinavyosema kuwa Kenya ina historia ya migogoro ya malipo ya fidia ya ardhi, ambayo itachelewesha ujenzi wa bomba hilo kutoka Lokichar hadi Lamu. “Hoja ya Uganda ni kwamba utafiti wa Tullow na CNOOC umesema malipo ya fidia ya ardhi ni suala kubwa litakalochelewesha ujenzi wa bomba kupitia kaskazini,” The Daily Nation limemkariri mmoja wa maofisa waliohudhuria mkutano huo.
Utafiti huo umetoa mfano migogoro mikubwa iliyokuwapo wakati wa kuchukua ardhi kwa ajili ya ujenzi wa bomba wa Lamu Port Southern Sudan-Ethiopia Transport (Lapsset) na ujenzi wa reli ya viwango vya kimataifa (SGR).
Utafiti huo unaonya kuwa migogoro hiyo inaweza kusababisha kuongezeka kwa gharama kwa sababu wamiliki wa ardhi wana tabia ya kupandisha bei kunapokuwa na miradi.
Uganda pia imedai utafiti umeonyesha maeneo ambayo bomba litapitia hayana barabara nzuri na hivyo hilo litakwamisha ujenzi, hali kadhalika bandari ya Lamu bado haijajengwa na inaweza kuwa haijakamilika ifikapo mwaka 2018 wakati Uganda itakapokuwa tayari kuanza kusafirisha nje mafuta.
Utafiti huo umeishauri Uganda ikubaliane na Tanzania, ambayo bandari yake ya Tanga inahitaji marekebisho madogo.
Lakini Kenya iliihakikishia Uganda kuwa suala la vikwazo vya malipo ya fidia halitachelewesha ujenzi wa bomba na kwamba ujenzi wa reli unaendelea baada ya wamiliki wa ardhi kufidiwa. Kenya pia ilisema ujenzi wa barabara pembeni ya Lapsset unaendelea.
Ujumbe wa Kenya pia ulikihakikishia kikao hicho kuwa mara ujenzi wa bomba hilo utakapokamilika, itahakikisha linalindwa, ikitoa mfano wa bomba la mafuta kutoka Mombasa hadi Eldoret.
“Kuhusu mashambulizi ya kigaidi, hatua za kutosha zimechukuliwa. Kwanza tishio la ugaidi liko kwenye nchi zote za Afrika Mashariki,” ofisa wa Wizara ya Nishati alikaririwa na Daily Nation.
Waandishi wa Kenya wanasikitika mradi huo kutekwa na Tanzania.
“Njia ya Tanzania sasa inaweka ushindani mpya kwa usafirishaji wa baadaye wa mafuta kutoka nchi nyingine za maziwa makuu, hasa mashariki ya Congo DR na Sudan Kusini,” linaandika Daily Nation
Mwandishi wa kujitegemea wa Uganda, Angelo Izama aliandika katika barua yake ya wazi kwa Rais Museveni kuwa kupitishia bomba hilo Tanzania kuna faida kwa Waganda.
“Njia mbadala ya bomba kwenda Tanga itatupa nafasi ya kufikia bandari mpya na kupanua wigo wa biashara na Tanzania,” anaandika Izama katika barua hiyo aliyoichapisha kwenye tovuti yake.
“Hii itajumuisha kuagiza na kuuza nje gesi asilia ya Tanzania ambayo Uganda inaihitaji kwa ajili ya unafuu katika gharama za kupikia
.”   

Mchezaji wa Sunderland, Adam Johnson ahukumiwa miaka sita jela baada ya kujihusisha kimapenzi na binti wa miaka 15.Fahamu zaidi hapa.

 Mchezaji wa mpira wa miguu, Adam Johnson amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela baada ya kukutwa na hatia ya kufanya mapenzi na binti wa miaka 15.

Mchezaji wa Sunderland, Adam Johnson ahukumiwa miaka sita jela baada ya kujihusisha kimapenzi na binti wa miaka 15

Mchezaji wa mpira wa miguu, Adam Johnson amehukumiwa kifungo cha miaka sita jela baada ya kukutwa na hatia ya kufanya mapenzi na binti wa miaka 15.
johnson
Jaji alimwambia kuwa hajaonesha majuto yoyote kutokana na kitendo chake na ni makosa yake mwenyewe
“This will be your first prison sentence, this is all entirely your fault.”
Mchezaji huyo ambaye alikuwa analipwa pound 60,000 kwa wiki ataanza kutumikia kifungo chake leo baada ya kuhukumiwa na jaji Jonathan Rose.

Babu Tale Atoboa Siri...Diamond Alishawahi Kumtoa Damu Chid Benzi na Kumuwekea Damu Safi ili Aache Madawa ya Kulevya.Fahamu zaidi hapa.

Meneja wa wanamuziki wa bongo fleva Babu Tale ameweka wazi kitu ambacho watu wengi walikuwa hawakijui kuhusu Diamond na Chid Benz.

Akiongea kwenye kipindi cha eNews kinachorushwa na East Africa Television, Babu Tale ameweka wazi kuwa Diamond Platnums ambaye anamsimamia, alishawahi kumsaidia Chidi Benzi kuacha madawa, kwa kwenda kumtoa damu na kumuwekea damu safi, lakini jambo hilo lilikuwa la siri ndio maana aliweza kurudia.

"Diamond alimshamtoa Chidi damu, kutoa ile yenye madawa, lakini alirudia unajua Chid anaacha na kurudia, sasa labda ndio maana ilikuwa rahisi kwa yeye kurudi kwa sababu ilikuwa siri, Damond siku hiyo alishinda hospitali kutwa nzima, akimtoa Chidi damu", alisema babu tale.

Kwa sasa Chid Benzi amepelekwa Rehab bagamoyo baada ya kurudia matumizi ya madawa ya kulevya, na kumuathiri kwa kiasi kikubwa, na ameahidi kuacha matumizi ya madawa hayo

Director Nisher; Nini Kimepoteza Umaarufu Wa Kazi Zake.Fahamu zaidi hapa.

Director nisher nakumbuka kipind kile unafanya Mama Yeyo, Jikubali, na Nje ya box. Kila mtu anayependa muziki mzuri basi sio rahisi kukosa kulitaja jina lako ukipost kipande cha video tu insta watu wanakurupusuana kila kona waje wakiangalie Video zako zilibamba sana mpaka kupigwa channel 0 Wasanii wote walikuwa wanakuja chuga kupata huduma yako.

Mambo yalivyo sasa: Nisher huna fans yaan umebaki kama gofu, watu wanamuamini Hanscana, Khalfan, na Joowzey wanakuacha wewe, nimepita jana Youtube Video yako ya mwisho ina viewers elfu 12, nini tatizo? Ndo kusema baba ako (Geordavie) hapendi unachofanya? ulilewa sifa ulipokuwa on top? au ndo Hanscana na Khalfan wamekufunga kwenye chupa?

Thursday, 24 March 2016

#YALIYOJIRI>>>Walinzi Watatu wa Suma JKT Watiwa Mbaroni Kwa Wizi wa Kompyuta 50 Chuo Kikuu cha Dodoma ( UDOM ).Fahamu zaidi hapa.

Walinzi watatu wa Suma JKT na askari mmoja wa Kituo  Kikuu cha Polisi Mkoa wa Dodoma, wametiwa mbaroni kwa tuhuma za wizi wa kompyuta zinazokadiriwa kufikia 50 mali ya Chuo Kikuu Dodoma (Udom).

Chanzo chetu cha habari kilieleza kuwa wizi huo ulitokea juzi baada ya chuo hicho kufungwa kwa ajili ya mapumziko ya Sikukuu ya Pasaka.

Inadaiwa kuwa katika wizi huo baadhi ya walinzi wa Suma JKT ambao wanajukumu la kulinda chuo hicho, walihusika huku watatu wakishikiliwa na polisi.

Hata hivyo, chanzo hicho kilieleza kuwa baadhi ya askari wa Kituo Kikuu cha Polisi Dodoma wanadaiwa kuhusika na kuzua mkanganyiko katika uchunguzi wa tukio hilo.

“Katika wizi huo, pia kuna  askari kutoka mjini ametajwa na walinzi wa Suma JKT kuhusika, sasa baada ya kupata taarifa hizo ndiyo wanafanya mpango wa kumkamata,” kilisema chanzo hicho cha habari.

Ofisa Habari wa Udom, Beatrice Baltazar jana alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo na kwamba, bado hawajajua idadi kamili ya kompyuta zilizoibiwa.

“Ni kweli kuna wizi wa kompyuta hapa chuoni, lakini sijajua idadi kamili ya kompyuta zilizoibwa, ila kuna walinzi watatu wa Suma JKT wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano,” alisema Beatrice.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa naye alithibitisha kuwapo kwa taarifa za tukio hilo, lakini hakuwa tayari kuzungumzia kwa undani kwa kuwa yupo likizo.

Hata hivyo, Mambosasa alikanusha kuwa hakuna polisi aliyehusika katika tukio hilo bali ni walinzi wa Suma JKT.

“Hakuna askari wetu aliyehusika katika tukio hilo, wenye jukumu la kulinda chuo hicho ni Suma JKT ndiyo wanaoshikiliwa kwa mahojiano zaidi,” alisema Mambosasa.

Wednesday, 23 March 2016

Download nyimbo ya tiwa-savage-feat-wizkid "bad".Hapa hapa.


Download nyimbo ya soggy-doggy-nimemiss-kukabwa.Hapa hapa.


Download nyimbo ya Lady Jaydee inayoitwa "Ndi Ndi Ndi".Hapa hapa.


TFF YAPIGA MARUFUKU KUCHEZA MCHEZO WA KUBAHATISHA(BETTING).FAHAMU ZAIDI HAPA.

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inapenda kuwakumbusha wanafamilia wa mpira wa miguu kuto kushiriki katika michezo ya kubahatisha (Betting)juu ya ibara ya 59 kifungu kidogo cha 11 kinachotamka:
TFF Family members shall at all times comply with the following ethical principles "To not take part in betting connected with football and do not tolerate any form of manipulation or unlawful influencing of match results".

Hivyo wanafamilia ya mpira wa miguu Tanzania wanakumbushwa kuheshimu Katiba ya TFF Kwa kutoshiriki katika michezo ya kubahatisha (betting).

Wanafamilia ya TFF ni pamoja na viongozi wa mpira wa ngazi, zote, wachezaji, makocha, waamuzi, makamisaa, waajiriwa wa TFF, wajumbe wa kamati mbali mbali za TFF na wengine wote ambao kwa namna moja au nyingine wanajihusisha na mpira wa miguu

#YALIYOJIRI>>>> MSTAHIKI MEYA MANISPAA YA KINONDONI AZINDUA RASMI UGAWAJI WA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAWAKE NA VIJANA.FAHAMU ZAIDI HAPA.

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akizindua rasmi ugawaji wa fedha za Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana katika Kata 6, kati ya Kata 34 Manispaa hiyo ya Kinondoni mapema jana.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob leo amezindua rasmi ugawaji wa fedha za Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana katika Kata 6, kati ya Kata 34 zinazotarajia kupata Tsh 200,000,000/= kila Kata ifikapo julai, 2016.

Hadi sasa Manispaa ya Kinondoni imepeleka katika Benki ya wananchi ya Dar es Salaam, (DCB) Jumla ya Tsh 855,003,614017 kwa ajili ya mikopo ya wanawake na vijana ambapo ifikapo julai 2016 ambao ni mwisho wa Mwaka wa fedha 2015/2016 zitafikia zaidi ya Tsh 4.5 billion ambayo ni sawa na asilimia 10% ya mapato ya ndani ya Manispaa ya Kinondoni kwa mujibu ya magizo ya Bunge.

Benki ya wananchi wa Dar es salaam,Tawi la Magomeni imefungua vituo 36, vya kuratibu shughulii za Mikopo ya vikundi vya wanawake na vijana katika maeneo mablimbali ya Kata za Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ili kuwarahisishia wananchi kupata huduma za mikopo hiyo kwa karibu.

Vikundi vilivyonufaika katika uzinduzi wa leo na kiasi cha fedha kilichotolewa:-
Stopover tsh 8,750,000/= kwa ajili ya biashara ya sabuni za Maji na Miche
Makabe tsh 5,250,000/= kwa ajili ya biashara ya utengenezaji wa sabuni na uuzaji wa Mkaa.
Mbezi luis, Tsh 7,000,000/= kwa ajili ya Nursery School, Tigo pesa, Mpesa.

Kilungule tsh 2,000,000/= kwa ajili ya Biashara ya Mitumba, genge na Saloon.
Kigogo tsh 10,000,000/=kwa ajili ya biashara ya Mama lishe, Saloon ya Kike na Kiume.

Aidha Mstahiki Meya amewataka wanawake na Vijana kujitokeza kwa wingi ili wapatiwe mafunzo na kupewa Mikopo kwa fedha zilizopo Benki na zile zinazoendelea kupelekwa kwa lengo la kuwawezesha wanawake na vijana kupata mikopo kwa utaratibu wa kuwashirikisha viongozi na watendaji ngazi ya Mitaa na Kata.
Imetolewa na:-
MSTAHIKI MEYA
MANISPAA YA KINONDONI
23/03/2016.
 Baadhi ya washiriki wakiifuatilia uzinduzi huo wa ugawaji wa fedha za Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana katika Kata 6, kati ya Kata 34 Manispaa hiyo ya Kinondoni mapema jana.

 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akikabidhi moja ya hundi hiyo
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akikabidhi moja ya hundi hiyo
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh. Boniface Jacob akikabidhi moja ya hundi hiyo zilizozinduliwa rasmi wa ugawaji wa fedha za Mikopo ya Mfuko wa wanawake na vijana katika Kata 6, kati ya Kata 34 Manispaa hiyo ya Kinondoni mapema jana.

LADY JAY DEE AJIBU TETESI ZA KURUDIANA NA GARDNER G HABASH.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Msanii mkongwe katika muziki wa bongo fleva, Lady Jaydee amefunguka kuhusiana na tetesi kwamba amerudiana na aliyekuwa mume wake Gadner G Habash.

Aliulizwa swali hilo na mtangazaji Sam Misago katika kipindi cha E News kinachorushwa na kituo cha EATV kila siku ya Jumatatu hadi Ijumaa.
“Watu wengi walinipenda kama nilivyo na hawakunipenda nikiwa na mtu yoyote, sipendi kuelezea mambo yangu binafsi nawaomba watanzania wanipende kama mimi kama Jaydee na si vinginevyo,”alisema Jaydee.
Msanii huyo ameibuka tena na wimbo mpya unaokwenda kwa jina la Ndindindi ambapo amesema video yake ataitoa itakapokuwa tayari.

CHANZO na Bongo5.


Mbwana Samatta aibeba Taifa Star's baada kuifungia goli moja.Fahamu zaidi hapa.

Mbwana Samatta wakiwa katika pozi la fura na kiungo wa Simba  na timu ya taifa ya Tanzania Mwinyi Kazimoto baada ushindi wa bao moja lililofungwa na Mbwana Samatta baada ya Mbwana Samatta dk 30 kufuatia krosi ya Farid Mussa na kufanya matokeo kuwa FT Chad 1-0 Taifa Stars mpaka mpira unaisha.
 
Mwinyi Kazimoto ameionesha kwenye kupitia account yake ya facebook mbapo ameanfika ujumbe wenye kauli ya Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda ambayo kuna wakati aliitumia Bungeni na kauli hiyo ikapata umaarufu mkubwa sana ‘wapigwe’
.
Ongera sana Taifa Star's kwa ushindi.

Ic’u Ibrah amtaka Wema Sepetu kwa gharama yoyote ile, Ni baada ya kumalizana na Shamsa Ford.Fahamu zaidi hapa.

Nyota wa filamu Nchini Burundi na Rwanda Ibrahim Ismael ‘Ic’u Ibrah’ amefunguka kwa kusema kuwa moja kati ya ndoto zake ni kuigiza filamu moja kubwa na Madame Wema Sepetu kwani ni msanii anayeamini kuwa ni mwigizaji mzuri na anaweza kuigiza.

“Nashukru kwa mara ya kwanza kuigiza na actress kutoka Tanzania Shamsa Ford, lakini nitafurahi sana nitakapofanikiwa kuigiza na Wema Sepetu kwa gharama yoyote, anajua sana mimi ni kama Kanumba vile,”anasema Ibrah.
 
Msanii huyo nyota raia wa Burundi amedai kuwa anazikubali sana kazi za marehemu Steven Kanumba huku akiamini kuwa msanii huyo alikuwa bora kwa Tanzania anatamani awe kama Kanumba katika uigizaji na hilo anaamini kuwa atalifanya.
 
Ibrah ni mwigizaji na mtayarishaji wa filamu nchini Burundi na tayari amefanikiwa kutayarishaji na kuigiza filamu kali na za kusisimua kama vile Wife of my Life, Fake deal, Seconde na Questions House ambazo zimeteka soko la filamu Burundi, Rwanda, Congo DRC na sehemu nyingine.
 
Pia msanii huyo amefanikiwa kuigiza filamu na msanii wa Swahilihood Shamsa Ford inayoitwa Najuta Shamsa itakayosambazwa Bongo ikishirikisha wasanii wengine wakali wa filamu kutoka Burundi kama Angel, Anir chini ya Wise muongozaji na mtayarishaji wa filamu hiyo

#YALIYOJIRI>>>>Wananchi Mwanza waandamana kupinga kuuzwa kwa Mlima wa Buyombe.Fahamu zaidi hapa.

Mamia ya wakazi wa mtaa wa Buyombe Kata ya Kahama jijini Mwanza wakiwa na silaha za jadi,wameandamana kupinga vikali kuuzwa kwa Mlima wao kunakodaiwa kufanywa na baadhi ya watumishi wa idara ya ardhi na mipango miji ya jiji hilo kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya chuo cha elimu ya biashara,kampasi ya Mwanza huku baadhi yao wakionyesha hasira zao baada ya kuanza kung’oa vigingi vyote pamoja na mabango ya Chuo hicho.

Wakazi hao wanasema kuwa hawako tayari kuchangia shilingi elfu hamsini kwa kila kaya kwa ajili ya ujenzi wa shule yao ya msingi kwani zaidi ya shilingi milioni mia sita zilizotokana na mauzo ya mlima huo kwa chuo cha elimu ya biashara kampasi ya Mwanza pamoja na wananchi wengine zinatosha kabisa kugharimia miundombinu ya huduma za kijamii kama vile shule,zahanati,maji ya bomba na Barabara.

Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Buyombe,Emanuel Zambezi amesema madai ya wakazi hao yana mantiki kubwa.

AY na Prezzo wasababisha mapenzi ya Dayna Nyange na mchumba wake yavunjike.Fahamu zaidi hapa.

Msanii wa Bongo Fleva, Diana Nyange ‘Dayna’, amesema kilichosababisha wakaachana na mchumba wake ni wivu wa mapenzi uliotokana na picha aliyopiga na wasanii wawili wa Kenya, Wahu na Prezzo pamoja na Mtanzania, Ambwene Yessaya ‘AY’.

Dayna anasema picha hiyo alipiga na wasanii hao kabla hajawa maarufu wala kujihusisha na muziki kwa kiasi kikubwa hivyo hiyo ilikuwa sehemu ya kutafuta marafiki wa kumsaidia kimuziki.

“Kutokana na picha hiyo mchumba wangu huyo alihisi kwamba mmoja wa wasanii hao labda natoka naye kimapenzi hivyo akawa hataki nipige picha na wasanii na nisijihusishe tena na masuala ya kimuziki.

“Muziki ni kitu ninachokipenda sana katika maisha yangu hapo nikaona wivu umezidi kwa mwezangu ambaye tumebarikiwa kupata mtoto mmoja wa kike mwenye miaka 10, tukaamua kuachana nami nikaendelea na muziki wangu hadi leo bila mchumba, mpenzi wala nini na maisha yanaenda,” alijieleza mrembo huyo.

Dayna alianza kujulikana katika muziki mwaka 2008 baada ya kuimba wimbo wa ‘Mafungu ya Nyanya’ na msanii aliyewika katika kampeni ya urais na wabunge mwaka 2005, Marlow, kisha akatoa ‘Nivute kwako’ na sasa anatamba na wimbo wa ‘Ungejua’.

Monday, 21 March 2016

#YALIYOJIRI>>>Lucy Mayenga Ajisalimisha....Amuomba Rais Magufuli Ampumzishe Ukuu wa Wilaya.Fahamu zaidi hapa.

Wakati Taifa likisubiri uteuzi wa wakuu wa wilaya huku wanaoshikilia nafasi hizo wakiwa katika chekeche kwa kuzingatia vigezo vitano, Mkuu wa Wilaya Iramba, mkoani Singida, Lucy Mayenga amemuomba Rais John Magufuli asimjumuishe kwenye orodha ya wakuu hao anayotarajia kuitangaza wakati wowote.

Rais Magufuli ameweka bayana vigezo atakavyotumia kufanya uteuzi wa wakuu hao wa wilaya ambavyo ni pamoja na suala la migogoro ya ardhi, tatizo la elimu hasa upungufu wa madawati, njaa na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu alivyovitangaza wakati akizungumza na wazee wa Dar es Salaam na katika uteuzi wa wakuu wa mikoa, alizungumzia pia suala la wafanyakazi hewa ambao wamekuwa wakilipwa mishahara bila ya wahusika kuchukua hatua kudhibiti.

Akizungumza kwenye kikao cha UWT, Mkoa wa Shinyanga mwishoni mwa wiki, Mayenga ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalumu alisema aliwasilisha ombi hilo binafsi kwa Rais Magufuli ili apate fursa ya kusimamia biashara zake alizosema zinazodorora kutokana na kubanwa na majukumu ya ukuu wa wilaya.

“Pamoja na ukuu wa wilaya, mimi pia ni mbunge na wakati huohuo ni mfanyabiashara; haya ni majukumu mengi kutekelezwa na mtu mmoja kwa wakati moja,”alisema Mayenga 

Aliwaambia wajumbe waliohudhuria mkutano huo uliofanyika katika Kata ya Nyamilangano, wilayani Ushetu kuwa biashara zake nyingi zilizopo mkoani Shinyanga zimedorora kutokana na kukosa usimamizi wake.

“Ombi hili nililitoa binafsi kwa Waziri Mkuu ambaye alinishauri kusubiri uteuzi; isitafsiriwe kwamba nimeogopa kasi ya utendaji ya Serikali ya Awamu ya Tano.Hapana! Nimeona ni vyema nibaki na ubunge na biashara zangu,” alisema Mayenga ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari.

Baadhi ya wanachama wa UWT waliohudhuria mkutano huo walimpongeza kwa uamuzi huo wakisema unapaswa kuigwa na viongozi wengine wenye majukumu mengi kwa kuachia watu wengine nafasi za kutumikia umma badala ya kung’ang’ania nafasi zote.

“Nampongeza Mheshimiwa Mayenga kwa uamuzi wake wa kuomba asiteuliwe tena kwenye nafasi ya ukuu wa wilaya kwa sababu itatoa fursa kwa watu wengine kutumikia nafasi hiyo,” alisema Selina Mkula.

Katika mkutano huo ambao Mbunge wa Ushetu, Elias Kwandikwa alitoa msaada wa mifuko 60 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa madarasa katika shule za msingi Nyamilangano na Mitonga pamoja na Shule ya Sekondari Kisuke, wanachama wapya 55 walijiunga na UWT.

Mbunge huyo pia aliahidi kutoa vyerehani 20 kwa makatibu kata wa UWT ili kusaidia harakati za maendeleo ya wananchi kwa kuanzisha vikundi vya kiuchumi katika kata zao.