Home »
Habari Moto
» AY na Prezzo wasababisha mapenzi ya Dayna Nyange na mchumba wake yavunjike.Fahamu zaidi hapa.

Msanii wa Bongo Fleva, Diana Nyange ‘Dayna’, amesema kilichosababisha
wakaachana na mchumba wake ni wivu wa mapenzi uliotokana na picha
aliyopiga na wasanii wawili wa Kenya, Wahu na Prezzo pamoja na
Mtanzania, Ambwene Yessaya ‘AY’.
Dayna anasema picha hiyo alipiga na wasanii hao kabla hajawa maarufu
wala kujihusisha na muziki kwa kiasi kikubwa hivyo hiyo ilikuwa sehemu
ya kutafuta marafiki wa kumsaidia kimuziki.
“Kutokana na picha hiyo mchumba wangu huyo alihisi kwamba mmoja wa
wasanii hao labda natoka naye kimapenzi hivyo akawa hataki nipige picha
na wasanii na nisijihusishe tena na masuala ya kimuziki.
“Muziki ni kitu ninachokipenda sana katika maisha yangu hapo nikaona
wivu umezidi kwa mwezangu ambaye tumebarikiwa kupata mtoto mmoja wa kike
mwenye miaka 10, tukaamua kuachana nami nikaendelea na muziki wangu
hadi leo bila mchumba, mpenzi wala nini na maisha yanaenda,” alijieleza
mrembo huyo.
Dayna alianza kujulikana katika muziki mwaka 2008 baada ya kuimba wimbo
wa ‘Mafungu ya Nyanya’ na msanii aliyewika katika kampeni ya urais na
wabunge mwaka 2005, Marlow, kisha akatoa ‘Nivute kwako’ na sasa anatamba
na wimbo wa ‘Ungejua’.
Related Posts:
#YALIYOJIRI>>>>>Kauli ya CHADEMA Kuhusu Hatua za NHC na Rasilimali za Mwenyekiti Mbowe.Fahamu zaidi hapa.
Kutokana na habari zilizoandikwa leo na vyombo vya habari mbalimbali
nchini kuhusu tukio la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kupitia kwa
madalali wake 'kuvamia' jengo lenye rasilimali za Mwenyekiti wa CHADEMA
Taifa, Free… Read More
#YALIYOJIRI>>>CHADEMA Wagoma Kuhamia Dodoma, Wadai Hawana Mpango Huo.Fahamu zaidi hapa.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema wazo la kuhamia Dodoma halimo kwenye ajenda zake.
Akizungumza na Mwananchi hivi karibuni, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk
Vincent Mashinji alisema chama hicho hakina mpango… Read More
#YALIYOJIRI>>>Taarifa Ya Jeshi La Ulinzi La Wananchi Wa Tanzania Kufuatia Habari Iliyoandikwa Kwenye Gazeti La Tanzania Daima.Fahamu zaidi hapa.
Jeshi
la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania limesikitishwa na taarifa iliyotolewa
na gazeti la Tanzania Daima toleo Nambari 4290 la tarehe 01 Septemba
2016, ikihusisha shughuli za Jeshi hilo zinazoendelea katika maadhimisho… Read More
#YALIYOJIRI>>>>>Rais Magufuli Awasili Pemba Kwa Ziara Ya Kikazi Ya Siku Mbili.Fahamu zaidi hapa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Asubuhi ya
leo tarehe 02 Septemba, 2016 amewasili Kisiwani Pemba ambapo majira ya
Alasiri anatarajiwa kuzungumza na wananchi wa Pemba katika Mkutano wa
h… Read More
#YALIYOJIRI>>>>Waziri Mkuu Majaliwa Akwama Kuhamia Dodoma.Fahamu zaidi hapa.
SERIKALI Mkoa wa Dodoma imesema Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa atahamia
rasmi mkoani humo mara baada ya kumalizika kwa vikao vya Bunge
vinavyoanza wiki ijayo, Septemba 6.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana alisema ba… Read More
0 comments:
Post a Comment