Mkuu
wa mkoa wa Dar es salaam amekutana na Kamanda wa Polisi kanda maalum
Simon Sirro pamoja na Askari Polisi kwa lengo la kujionea mwenendo wa
jeshi hilo ambapo wamekubaliana kutoa zawadi ya milioni moja kila baada
ya miezi mitatu kwa kila Askari Polisi aliyepambana na majambazi.
"Askari
wetu wanafanya kazi katika mzangira magumu na wanachangamoto kubwa.
Nmeona nitengeneze mfumo wa kuwapa motisha, kwahiyo nimeongea na Kamanda
Sirro nimemuambia kuwa kila askari atakayeonekana amefanya vizuri mimi
kama mkuu wa mkoa nitakuwa na zawadi ya milioni moja kwake kama motisha.
"Kuna
watu wengi wana silaha halali na wengine wanamiliki isivyo halali,
kwahiyo tumekubaliana kuanzia leo hadi tarehe 1 aprili 2016 tunawaomba
wana Dar es salaam wote waende kwenye ofisi za polisi kutoa taarifa za
uhalali wa silaha zao.
"Tunataka kujihakikishia tunazo silaha ngapi katika mkoa wetu maana kuna wengine wanazitumia kinyume cha taratibu.
"Sasa
olewako tukukute unamiliki silaha, tunahitaji kuliona jiji letu la Dar
es salaam linaongoza kwa amani, hatutaki kuona majambazi wakipora kwenye
mabenki wala kuwapora watu kwa silaha." Amesema RC Paul Makonda
0 comments:
Post a Comment