Dereva na mtuhumiwa raia wa Msumbi akiwa chini ya ulinzi
Sehemu ya 'mzigo' huo
Askari polisi akichana tenki la mafuta la gari hilo
Madawa
ya kulevya aina ya heroin yanayokadiriwa kuwa na thamani ya Rand za
Afrika Kusinu milioni 50 yamekamatwa yakisafirishwa ndani ya tenki la
mafuta la gari lililokuwa likielekea Gauteng kutokea Msumbiji.
Habari
zinasema hilo limetokea baada ya kikosi cha askari polisi wa mbwa cha
Whiteriver walifanikiwa kukamata madawa hayo baada ya kusimamisha gari
aina ya Toyota Prado lenye kutia mashaka katika geti la kulipia ushuru
wa barabara eneo la Nkomazi huko Mpumalanga siku ya Jumapili iliyopita.
Baada
ya upekuzi mbwa wa polisi alipata harufu katika moja ya matenki ya gari
hilo na kubweka kuwa mna 'mzigo', ndipo baada ya kufungua tenki hilo na
kulichana wakakuta 'unga' huo umefichwa ndani ya tenki hilo ukiwa
umefungashwa kwenye vifuko vya plastiki, alisema msemaji wa Polisi
Sajini Gerald Sedive.
"Madawa
ya kulevya yenye thamani ya R50 milioni yalikutwa kwenye tenki la
mafuta. Gari lilikuwa likitokea Msumbiji", alisema, na kuongezea kwamba
dereva wa gari hilo raia wa Msumbiji ametiwa mbaroni na hatua za
kisheria zitachukua mkondo wake.Chanzo Issa Michuzi Blog
0 comments:
Post a Comment