Spika
wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Mhe. Daniel Kidega (kulia) akitoa
taarifa ya Jumuiya hiyo mbele ya ya Wabunge wa Mabunge ya Afrika
Mashariki leo Jijini Dar es Salaam kuhusu masuala mbalimbali yanayoihusu
Jumuiya hiyo. Kushoto ni Mbunge wa Bungo hilo Mhe. Makongoro Nyerere.
Baadhi
ya Wabunge wa Mabunge ya Afrika Mashariki pamoja na waandishi wa habari
wakimsikiliza Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wakati akisoma
taarifa yake leo Jijini Dar es Salaam kuhusu masuala mbalimbali
yanayoihusu Jumuiya hiyo.
NCHI
wanachama wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) wameaswa kuenzi lugha ya
Kiswahili na kuifanya kuwa lugha ya kufanyia kazi katika Jumuiya hiyo.
Hayo
yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Spika wa Bunge la Afrika
Mashariki, Mhe. Daniel Kidega alipofanya Mkutano uliowahusishwa Wabunge
wa Mabunge ya Afrika Mashariki (EALA) lengo likiwa kujadili masuala
mbalimbali yanayohusu Jumuiya hiyo.
Mhe.
Kidega ameeleza kuwa, lugha ya Kiswahili ina umuhimu mkubwa kwa Jumuiya
hiyo ambapo ameshauri kuwa kuna haja ya kupitia katika Sheria ya Bunge
hilo ili kuhakikisha kuwa Kiswahili na Kiingereza vinatumika ama
kuzungumzwa kila mahali katika Afrika Mashariki.
‘’Tupate
muda wa kutumia Kiswahili na kuhakikisha kuwa Kiswahili kinazungumzwa
katika nchi zote za Afrika Mashariki kwani ni lugha ya Afrika na sisi ni
Waafrika, hivyo tutafute namna ya kukifanya Kiswahili kuwa lugha ya
kufanya kazi kwa Jumuiya yetu ya Afrika Mashariki,’’ alisema Kidega.
Aidha,
Spika Kidega amegusia suala la watu wenye ualibino ambapo ameeleza
kuwa, nchi wanachama hazinabudi kupiga vita masuala ya ukatili kwa watu
wenye ualbino ambapo amezitaka Serikali wanachama wa Jumuiya hiyo
kuhakikisha kuwa Albino wanaheshimika kama binadamu wengine na
kuwachukulia hatua kali za kisheria wahusika wanaojihusisha na ukatili
dhidi ya watu hao, kwani kwa kufanya hivyo kwa pamoja kutapunguza ama
kuondosa changamoto zinazowakabili watu wenye ualbino.
Mhe.
Kidega hakusita kuwapongeza Wabunge wanachama wa EALA waliohudhuria
Semina ya Siku mbili (3 Machi- 4, 2016) iliyolenga kujadili masuala ya
changamoto za uchaguzi kwa nchi za Afrika Mashariki ambapo waliweza
kujadili kwa undani baadhi ya changamoto za uchaguzi na madhimio
mbalimbali yenye kuleta maendeleo katika Jumuiya hiyo.
Kwa
upande mwingine, Mhe. Kidega amewaasa Wazanzibar ambao hivi karibuni
wanaenda kupiga kura na kuwataka kufanya uchaguzi huo kwa uhuru na haki
ikiwemo kudumisha amani ya Kisiwani humo pamoja na Tanzania kwa ujumla.
‘’Niwaombe
Wazanzibar ambao mda si mrefu mnaenda kurudia uchaguzi wenu, tiini
sheria za nchi, jitokezeni kupiga kura kwa wingi na hakikisheni kuwa
mnafanya uchaguzi wenu kwa uhuru na haki ili kudumisha amani ya
Tanzania, alisema Kidega.
Mhe.
Kidega pia amewapongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
John Pombe Joseph Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya ambayo
inabadilisha sura ya Tanzania pamoja na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa kwa kujituma kwao
katika kuwatumikia watanzania wote.
0 comments:
Post a Comment