Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akishuka kutoka katika kivuko cha Mv Kilombero mara baada ya kukagua utendaji kazi wa Nahodha wa kivuko hicho.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. MAKAME MBARAWA amesema
Serikali imejipanga kuhakikisha ujenzi wa daraja la mto Kilombero
unakamilika ifikapo mwezi Novemba mwaka huu ili kumaliza changamoto ya
usafiri inakabili wanachi wa wilaya za KILOMBERO na ULANGA mkoani
MOROGORO.
Prof.
MBARAWA ametoa kauli hiyo Wilayani KILOMBERO mkoani MOROGORO mara baada
ya kukagua maendeleo ya kivuko cha MV- KILOMBERO kilochokuwa
kikikarabatiwa kufuatia kuzama mwishoni mwa mwezi Januari ambapo amesema
tayari Serikali imemlipa mkandarasi zaidi ya shilingi bilioni kumi na
moja ili kuhakikisha ujenzi wa daraja katika mto huo linakamilika kwa
wakati.
Amesema tayari mkandarasi anayejenga daraja hilo kutoka China
ameshalipwa shilingi bilioni 11.2 katika kipindi cha wiki mbili
zilizopita ambapo hivi sasa kazi inayoendelea kwa mkandarasi huyo ni
kutengeza vifaa maalumu kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo huko nchini
China .
“ Ifikapo novemba mwaka huu tutakuwa tumelipatia ufumbuzi wa
kudumu swala la daraja la Kilombero na hivyo mpapita kwa uhakika na
kufanya biashara zenu kwa uhakika”, amesema Prof.MBARAWA.
Aidha Prof. Mbarawa amekagua na kuruhusu kuanza tena kwa shughuli
za usafirishaji katika kivuko cha Mv Kilombero ambazo zilikuwa
zimesimama kwa takribani kipindi cha mwezi mmoja tangu kivuko hicho
kupata ajali mnamo Januari mwaka huu kufuatia mvua kubwa iliyoambatana
na upepo.
Ukabati wa kivuko hicho umegharimu shilingi milioni 342.5 ambapo
Prof.MBARAWA amewataka wananchi kufuata maelekezo ya wasimamizi wa
kivuko wakati wa safari zao na kulipa nauli stahili.
“Lazima mlipe nauli kwa sababu nauli hiyo ndio tunayotumia
kuendeshea vivuko na pia mzingatie usalama wenu na kusikiliza maelekezo
ya wasimamizi wa kivuko ili kuepuka kadhia “amesisitiza Prof.MBARAWA.
Ujenzi wa daraja katika mto Kilombero ni sehemu ya mkakati wa
Serikali tangu awamu ya kwanza uliolenga kujenga madaraja makubwa ni
daraja la mto Rufiji mkoani Pwani, daraja Kirumi mkoani Mara, daraja la
Malagarasi mkoani Kigoma na Kigamboni la jijini Dar es salam.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akishuka kwenye kivuko cha MV KILOMBERO mara baada ya kukikagua.
Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa katikati akijadiliana jambo na Kaimu Mtendaji mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme nchini (TEMESA), Eng. Manase Ole Kujan kulia na mkuu wa wilaya ya Kilombero Lephy Gembe kushoto wakati akikagua kivuko hicho mara baada ya ukarabati.
0 comments:
Post a Comment