Friday, 18 March 2016

Jinsi ya Kuangalia kama Simu ni Feki.Fahamu zaidi hapa.

Hivi karibuni zilisambaa taarifa kwamba simu feki zote nchini Tanzania zitazimwa ifikapo mwezi Juni mwaka 2016, makala hii itakuonesha jinsi ya kuangalia kama simu yako ni feki ama la.

Hatukuweza kuthibisha moja kwa moja kwamba kweli simu zitazimwa mwezi Juni lakini tumejiridhisha kuwa kutakuwa na hatua dhidi ya wanaomiliki simu feki pindi itakapofika tarehe hiyo.

Zifuatazo ni hatua unazoweza kuzitumia kuangalia kama simu yako ni fake, hakuna mahitaji makubwa kufanya hili ila tu unahitaji simu yako unayoitumia na unayotaka kuiangalia.
Jinsi  ya angalia IMEI namba
  • Andika *#06# kisha bonyeza kitufe cha kupiga
  • Baada ya hapo simu yako itakuletea IMEI namba ambapo kama simu yako au kifaa chako kina laini mbili basi kutakuwa na IMEI namba mbili
  • Namba hii pia unaweza kuipata katika boksi la simu ama nyuma ya ya simu hiyo baada ya kutoa betri, utaijua kwa kuwa huwa ni tarakimu 15.
  • Nakili namba hizo pembeni.

Mfano wa IMEI namba iliyopatikana kwa kupiga *#06#
Jinsi ya kuangalia kifaa kama ni feki ama halali
  • Iandike ile namba uliyo nakili katika hatua iliyopita katika sehemu ya kuandikia ujumbe (SMS)
  • Utume ujumbe huo kwenda namba 15090
  • Baada ya kutuma meseji hiyo utaangaliziwa je hiyo IMEI namba ni ya simu ya aina gani na nani mtengenezaji wa simu hiyo.
  • Subiri majibu (haitachukua muda mrefu)
  • Ujumbe huo ukija unakuwa na maelezo ya kampuni iliyotengeneza simu hiyo pamoja na jina la simu hiyo.

Mfano wa ujumbe unarudishwa baada ya kutuma IMEI namba
Jinsi ya kujua kama simu yako ni feki
Kama jina la mtengenezaji wa simu yako pamoja na aina ya simu yako (Uliyo jibiwa baada ya kutuma IMEI namba) haviendani na majina ya simu yako (ambayo yameandikwa katika simu yako) basi ujue simu yako inamashaka na ni vyema kumuuliza muuzaji wako juu ya hilo.
Kama majina yaliyorudi hayaendani na majina yaliyoandikwa katika simu yako basi upo katika kundi lenye uwezekano wa kuwa na matatizo, TUNAKUSHAURI ufuate utaratibu na kuibadilisha ama kuacha kuitumia simu hiyo kabla ya mwezi Juni.
Kwanini TCRA wanataka tubadilishe simu

Simu isiyo na IMEI ni sawa na gari lisilo na namba za usajili {plate number}
Vyombo vya usalama vinaweza kukamata wahalifu wa kutumia mitandao ya simu kwa msaada wa IMEI namba hivyo mtu akiwa anatumia simu ambayo haina au ina IMEI namba ambayo sio sahihi anazuia utendaji kazi wa taasisi za usalama hivyo wao kama mamlaka wanatakiwa kuhakikisha kila mtu anatumia simu yenye IMEI namba sahihi.
Undelea kufuatilia Teknokona kwa habari mbalimbali katika lugha yako ya kiswahili.

Related Posts:

  • IGP Sirro: Tutamshughulikia Mange Kimambi. Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro amefunguka na kusema kuwa jeshi la polisi linatambua makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwanadada Mange Kimambi na kusema kuwa jeshi la polisi linashughulikia su… Read More
  • SOMA Nafasi za Ajira Zilizotangazwa Leo Jumanne. 16 Government Jobs Job Opportunity at CDM Smith, Finance and Accounting Manager Job Opportunity at CVPeople Africa, Secretary/Administrator Jobs at Meru University of Science and Technology (MUST) 2 Job Opportuniti… Read More
  • Wanajeshi wawili wa Tanzania wauawa Huko Kongo. Askari wawili wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania, wameuawa kwenye mashambulizi makali yanayoendelea nchini Kongo. Tukio hilo limetokea katika eneo la Beni ambako Askari wa Umoja wa Mataifa wa kulin… Read More
  • Mauzo ya Soko la Hisa Yazidi Kushuka. Mauzo ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), yameendelea kupungua hadi Sh1.5 bilioni Oktoba 6, kwa wiki ya pili sasa. Takwimu za DSE zinaonyesha wiki iliyoishia Septemba 22, mauzo ya soko hilo yalikuwa Sh53 bilioni ambay… Read More
  • Moto Mkubwa Wasababisha Maafa California, Marekani. Maeneo ya jimbo la California ambayo hukuza mizabibu yameathiriwa na moto mkubwa ambao unaenea kwa kasi sana na kusababisha vifo vya watu 10. Mamia ya watu wamehamishwa makwao na inakadiriwa kwamba zaidi ya nyumba 1,500 zi… Read More

0 comments:

Post a Comment