Raia wa Kichina kutoka kulia ni na Xu Fujie na Huang Jing ambao wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela au kulipa faini ya shilingi bilioni 54 leo katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Raia
wa China wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 au kulipa zaidi ya
sh.bilioni 54 kila mmoja kwa kukutwa na hatia ya makosa mawili.
Washitakiwa
hao katika kosa la kwanza ni kukutwa ni kuwa na nyara ya serikali ya
vipande vya meno ya tembo 706 yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni tano
na kosa la pili kushawishi kutoa rushwa kwa askari sh.milioni 30.
Washitakiwa hao ni Huang Jing pamoja na Xu Fujie wameanza kutumikia kifungo hicho leo baada ya kushindwa kutoa faini hiyo.
Akisoma
hukumu hiyo Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Sprian Mkeya
amesema kuwa kutokana na kupata maelezo katika pande zote mbili pamoja
na kuisababishia hasara serikali washitakiwa adhabu yao ni miaka 30 au
kulipa ya zaidi ya bilioni tano (5).
Hakimu Mkeya amesema washitakiwa hao wanaweza kukata rufaa makahakama kuu kutokana na hukumu iliyotoka.
Wakili
wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliomba mahakama iwape adhabu kali
kutokana na kosa waliolifanya na kudai kuwa kutokana na kukamatwa kwao
vitendo vya uhalifu kwa wanyamapori vimepungua
Kwa
upande wa Wakili upande wa washitakiwa Nehemia Mkoko aliomba mahakama
kuwaonea huruma kwa adhabu wataoipata ili waweze kutoka na kuweza
kujumuika na familia zao. Washitakiwa hao walikamatwa 2010 katika eneo la mikocheni mwaka huu.
Raia wa kichina wakisindikizwa na Askari Magereza mara baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela leo katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment