Naibu
Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi
Kigwangalla (kushoto) akiongozwa na Mganga Mfawidhi wa Zahanati ya
Msoga, Dk. Juliet Lema wakati wa ukaguzi huo. Kulia ni Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Pwani,Dkt. Beatrice Jane Byalugaba.
Serikali
kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeipa
hadhi ya kuwa Hospitali Wilaya iliyokuwa Zahanati ya Msoga ambayo
tayari imekamilisha jengo lake jipya la Hospitali hiyo inayotarajia
kuanza kuanzia Mwezi Aprili mwaka huu.
Akitoa
maagizo hayo baada ya ukaguzi wa timu ya wataalam kutoka Wizara hiyo ya
Afya pamoja na Naibu Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla waliofanya hivi karibuni katika Hospitali
hiyo, ameeleza kuwa kuanzia Mwezi Aprili ianze kazi kwa kuanza na
huduma za wagonjwa wa nje na baada ya miezi mitatu itaendeshwa na huduma
zote muhimu ikiwemo kulaza wagonjwa.
“Naagiza
ndani ya mwezi mmoja ianze kazi na huduma za kawaida. Baada ya miezi
mitatu itaendelea na huduma muhimu zote katika Hospitali hii mpya ya
Wilaya” alieleza Dk. Kigwangalla wakati wa kutoa hitimisho lake kwa
wasimamizi wa Zahanati hiyo ya Msoga.
Dk.
Kigwangalla na timu yake waliweza kukagua majengo ya Hospitali hiyo
mpya ambapo na kuona inakidhi vigezo ya kuwa Hospitali ya Wilaya.
Majengo
ya Hospitali hiyo yapo katika Kituo cha afya cha Msoga, kata ya Msoga,
Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani, Ni miongoni mwa Hospitali
itakayokuwa ya kisasa na kubwa.Aidha, kutokana na matukio mengi ikiwemo
ya ajali nyingi zinazotokea mara kwa mara katika barabara ya
Chalinze-Segera, Hospitali hiyo ya Wilaya itakuwa msaada na itawezesha
kupunguza mzigo wa vituo vya afya vya vya jirani ikiwemo Lugoba,
Chalinze na vinginevyo ndani ya Halmashauri hiyo yaa mji mdogo wa
Chalinze.
Jengo hilo la Hospitali ya Wilaya inavyoonekana kwa njeWaziri Dk. Kigwangalla akiwa na timu yake wakikagua eneo hilo la Hospitali ya Wilaya. Jengo linaloonekana nyuma awali lilipangiwa kuwa sehemu ya kuhifadhia maiti (Mochwari) hata hivyo wamebadilisha matumizi yake na Mochwari itajengwa mbali kidogo na hapo ilikutoa naafasi kubwa kwa kujengwa mochwari ya kisasa.
Dk.
Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni katika Zahanati ya Msoga mara
baada ya kufanya ukaguzi na kuagizia majengo mapya ya Hospitali hiyo
kuanzia mwezi ujao wa Aprili yaanze kutumika kama Hospitali ya Wilaya
ambapo Madawa na vifaa vinatarajiwa kupelekwa muda wowote kuanzia sasa.
0 comments:
Post a Comment