PAUL Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, ametangaza mpango mpya wa kuanzisha mtaa maalum utakaokuwa ukihusika na biashara ya uuzaji wa vinywaji vikali na baridi baa (bar).
Makonda
ameweka wazi mpango huo jana jijini Dar es Salaam ikiwa pia ndiyo siku
ambayo utekelezwa wa mpango wa walimu wa shule za msingi na sekondari
kusafiri bure kupitia usafiri wa umma (daladala) ulianza rasmi.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema mpango huo ni muendelezo wa ubunifu na uthubutu
wa mipango ya maendeleo ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa ukikosekana
miongoni mwa Watanzania na hivyo kufanya kasi ya maendeleo hapa nchini
kuwa ndogo tofauti na matarajio ya wananchi.
“Kinondoni
nina mpango wa kutengeneza mtaa mmoja maalum wenye bar tu ili watu
wakitaka kwenda kunywa pombe waende mtaa huo bila kubugudhiwa. Nasubiri
muda tu ufike kwa sababu haiwezekani kila eneo liwe na baa mpaka nyuma
ya misikiti na nyuma ya makanisa,” alieleza Makonda.
Wilaya
ya Kinondoni ndiyo wilaya yenye watu wengi zaidi hapa nchini ambapo kwa
mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 wilaya hiyo ina jumla
ya watu milioni 1.7 na kwasasa ikikadiriwa kufikia watu milioni 1.9.
0 comments:
Post a Comment