Saturday, 30 July 2016
#BURUDANI>>>>WANAMUZIKI WA DANSI WAMPIGA TAFU MAKONDA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
WANAMUZIKI wa Dansi nchini Jumamosi hii (leo) wanatarajia
kuungana na kufanya tamasha kubwa na la aina yake ambalo linategemewa
kuwa gumzo litakalofanyika katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni
jijini Dar.
Tamasha hilo ambalo limeandaliwa na Tanzania Band Festival, lina
malengo ya kumsapoti Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda katika
kampeni yake ya kuchangia madawati mashuleni kwani sehemu ya mapato ya
tamasha hilo yatakuwa kwa ajili ya kampeni hiyo.
“Tumeamua kushirikiana ili kumsapoti mkuu wetu wa mkoa Makonda
kwa namna anavyojitolea katika kuwasaidia wanafunzi lakini hata yeye
amekuwa akiusapoti Muziki wa Dansi,” alisema Said Mfaume mratibu mkuu wa
tamasha hilo.
Katika tamasha hilo kutakuwa na bendi kumi zitakazoshiriki
ambazo ni Msondo Ngoma,Sikinde, Mapacha wa Tatu,Yamoto Band, Banana
Zorro,Tip Top,Syklight, FM Academia na nyingine nyingi huku kiingilio
kikiwa shilingi 15,000 tu.
#MICHEZO>>>ANGALIA JOSEPH OMOG ALIVYOTUMIA WACHEZAJI 21 KWA MECHI MOJA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Kikosi cha Simba kilikuwa hivi:
1. Peter Manyika (out dk 72) / Vincent Angban
2. Besala Bukungu (out dk 45) / Hamad Juma
3. Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' (out dk 68) / Abdi Banda
4. Method Mwanjali
5. Novaty Lufunga (out dk 45) / Emmanuel Semwanza
6. Jonas Mkude (out dk 71) / Said Ndemla
7. Shiza Kichuya (out dk 79) / Peter Mwalyanzi
8. Mzamiru Yasin
9. Diauwo Johnson (out dk 45) / Mussa Ndusha (out dk 85) / Awadh Juma
10. Ibrahim Ajib (out dk 58) / Danny Lyanga
11. Jamal Mnyate (out dk 45) / Mohammed Ibrahim
Wafungaji:
Ibrahim Ajib dakika ya 20 akimalizia pasi ya Shiza Kichuya na Danny Lyanga dakika 69 akimalizia pasi ya Mohammed Ibrahim.
Blagnon hakucheza kocha alimpumzisha tu hakuwa na tatizo.
#MICHEZO>>>ALIYEONEKANA HANA KITU SIMBA, ACHUKUA TUZO YA MWANASOKA BORA WA RWANDA.FAHAMU ZAIDI HAPA.
Pierre ndiye mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Rwanda kwa msimu wa 2015-16.
Kwizera ameisaidia timu yake kubeba ubingwa wa Kombe la Amani ambalo bingwa wake hucheza michuano ya Kombe la Shirikisho.
Kiungo
huyo, alitimuliwa Simba baada ya kucheza nusu msimu tu huku mwenyewe
akilalamika kwamba Simba hawakumpa nafasi ya kucheza lakini wakatumia
muda mwingi kumlaumu.
Raia
huyo wa Burundi ambaye ni mtaratibu sana, alionyesha uwezo wa juu na
kuifanya Rayon ambayo ina mashabiki wengi zaidi nchini Rwanda kuwa timu
isiyokamatika hasa katika kiungo.
#MICHEZO>>>KILA USICHOKIJUA KUHUSU PAUL POGBA HIKI HAPA.
AMEFUNGA MABAO 7 YA MGUU WA KUSHOTO, 25 KULIA, KICHWA MAWILI NA UTAONA UKALI WAKE NDANI NA NJE YA BOKSI.
#YALIYOJIRI>>>>Kiwanda Maarufu Cha Dangote Chatozwa Faini Ya Shilingi Milioni 15 Kwa Uchafuzi Wa Mazingira.Fahamu zaidi hapa.
Serikali
kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC
limekitoza faini ya shilingi milioni 15, Kiwanda maarufu cha kutengeneza
simenti cha Dagonte Industry limited kilichopo mjini Mtwara kusini
mwa Tanzania, kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na
kanuni zake.
Katika
siku ya Pili ya Ziara ya ziara ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Mkoani Mtwara Imebainika
kuwa kiwanda hicho cha Dangote chenye muda wa miezi mitatu tangu kianze
kazi ya kutengenza siment, kimefanya uchafuzi wa mazingira kwa kukosa
sehemu maalum ya kuhifadhi taka katika kiwanda hicho, kutokuwa na
utaratibu mzuri wa kuhifadhi taka zitokanazo na makaa ya mawe kiwandani
hapo, kukosa vyoo kwa ajili ya matumizi ya wateja wao ambao ni madereva
na makondakta wanao chukua mzigo wa siment kiwandani hapo, na
kusafirisha kwenda sehemu mbali mbali za nchi, pamoja na kutokusakafia
sehemu ya nje ya kiwanda hicho ambapo imeelezwa kuwa eneo hilo la nje
wakati wa kipindi cha mvua mazingira yake huatarisha afya ya watumiaji
wa eneo hilo.
Kwa
Mujibu wa Naibu waziri Mpina, adhabu hiyo kwa kiwanda cha Dangote
inayotakiwa kulipwa ndani ya wiki mbili, inaenda sambamba na
urekebishaji wa kasoro hizo kiwandani hapo pamoja na kuhamsha uongozi wa
kiwanda hicho kwa kudharau sheria ya mazingira, na kutaka kiwanda hicho
kuajiri afisa mazingira ataeshughulia changamoto hizo.
Kwa
upande wake Meneja utumishi na utawala wa kiwanda hicho Bw. James
Kajeli aliomba serikali kusamehe adhabu hiyo kwani kiwanda kilikuwa
kwenye mpango wa kufanya marekebisho hayo na kuongeza kuwa kutokufanya
hivyo kwa wakati ni kujisahau kwa kibinadamu, na kuwa utengenezaji wa
baadhi ya miundombimu kiwandani hapo ulicheleweshwa na upatikani wa
baadhi ya vibali kutoka katika taasisi za serikali na si kudharau sheria
ya mazingira.
Naibu
waziri Mpina Pia alitembelea kiwanda cha kutengeneza gas cha Madiba na
kukisifu kwa utekelezaji wa sheria za mazingira na kuviasa viwanda vya
serikali, kuwa mfano katika kutii sheria za mazingira.
Ziara
ya Mhe. Mpina pia ilihusisha ukaguzi wa kiwanda cha kubangua korosho
cha micro mix cha mjini Mtwara, kiwanda cha gas cha Solvochemi pamoja na
fukwe ya mnazi bay iliyoathiriwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya
tabia nchi.
#YALIYOJIRI>>>Audio: Msikilize Rais Magufuli Akizungumzia Jinsi Atakavyoyapiga Mnada Majengo ya Serikali Dar na Atakachofanya Kwa Watumishi Watakaokataa Kuhama.Fahamu zaidi hapa.
Rais
John Magufuli amesema azma ya Serikali yake kuhamia Dodoma haraka
iwezekanavyo ipo pale pale huku akiwaonya wale wataong'ang'ania kubaki
Dar es Salaaam kuwa watakuwa wamejifukuzisha kazi wenyewe.
Alitoa msimamo huo mjini Singida jana kwenye mkutano wake wa kwanza wa hadhara tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka jana.
Alisema kuwa licha ya kuhamia Dodoma atahakikisha anauza majengo ya wizara mbalimbali yaliyopo Dar es Salaam kwa mnada ili wale wasiotaka kuhama,wahame kwa lazima.
Bonyeza Audio ya kwanza na ya Pili Kumsikiliza akiongea.
Alitoa msimamo huo mjini Singida jana kwenye mkutano wake wa kwanza wa hadhara tangu achaguliwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka jana.
Alisema kuwa licha ya kuhamia Dodoma atahakikisha anauza majengo ya wizara mbalimbali yaliyopo Dar es Salaam kwa mnada ili wale wasiotaka kuhama,wahame kwa lazima.
Sehemu ya Kwanza Sehemu ya Pili
Friday, 29 July 2016
#MICHEZO>>>>BIA YA KILIMANJARO RASMI YAAMUA KUACHANA NA SIMBA.Fahamu zaidi hapa.
Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), imeamua kutosaini mkataba wa kuendelea kuidhamini Simba.
Taarifa
kutoka ndani ya Simba, zinaeleza TBL imegoma kusaini mkataba ikionekana
kuingia hofu baada ya Yanga kutotaka kuendelea nao au waingie wakiwa na
ofa mpya.
“TBL wameona Yanga wanataka vitu vingi sana na kwao haitakuwa na faida, hivyo wameachana nao.
“Simba hawana shida, lakini watasaini vipi na Simba wakati kawaida zinatakiwa timu zote,” kilieleza chanzo.
“Hivyo wameamua kujiondoa na mkataba wao unaisha keshokutwa Jumapili.
“Sasa hili ni tatizo katika ulipaji mishahara kwa Simba maana lazima ugumu utaongezeka,” kilisisitiza chanzo.
Pamona
na hivyo imeelezwa kumekuwa na juhudi binafsi zinazofanywa na baadhi ya
viongozi kujaribu kuwashawishi TBL kupitia Kilimanjaro, wabadili
uamuzi.
#YALIYOJIRI>>>>CHADEMA wamjibu Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya tuhuma za kutumia matusi, uongo, uchochezi.Fahamu zaidi hapa.
Baada ya kulifanyia uchambuzi na
kulitafakari tamko la Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa, lililotolewa
jana na msajIli mwenyewe, Jaji Francis Mutungi tumeona ni jambo lenye
afya kwa ustawi wa demokrasia nchini, kusahihisha upotoshaji uliomo
katika taarifa hiyo ili kuendelea kumsaidia msajili na watu wengine,
watawala na walio sehemu ya utawala, kuelewa matakwa na maslahi ya
wananchi hasa katika wakati huu ambao taifa linapitia.
Kwa hakika tumeshangazwa na kauli
zilizotolewa na Msajili wa Vyama vya Siasa, ambaye pia ni Jaji wa
Mahakama Kuu, kutokana na jinsi ambavyo anaanza kuonesha kuyumba katika
kutimiza wajibu wake hasa kwa kutumia weledi na ujuzi wake wa sheria kwa
kiwango cha nafasi yake kama jaji.
Katika tamko lake alilolitoa jana na
kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari jana hiyo na leo, ameshindwa
kuonesha neno hata moja linaloashiria matusi, kashfa, uongo au hata
kuvuruga amani lililotolewa mbele ya waandishi wa habari juzi wakati
Chama kikisoma hadharani maamuzi ya kikao cha Kamati Kuu.
Ni jambo la kushangaza kuwa Msajili
Mutungi, Jaji wa Mahakama Kuu ameweza kuweka vifungu vingi vya kisheria
akidai kuwa vimevunjwa lakini hawezi kuonesha ushahidi wa namna
vilivyovunjwa au maneno yanayothibitisha kuvunja hizo sheria.
Hii si sahihi hata kidogo na inakuwa ‘serious’ zaidi inapofanywa na mtu mwenye weledi wa sheria wa kiwango cha Jaji Mutungi.
Hii si sahihi hata kidogo na inakuwa ‘serious’ zaidi inapofanywa na mtu mwenye weledi wa sheria wa kiwango cha Jaji Mutungi.
Wakati Jaji Mutungi akinukuu vifungu vya
sheria na kanuni akionekana dhahiri kuwa kuegemea na kuwatetea watawala
ambao wamedhihirisha kuwa wanatamani nchi irudi enzi za ‘ujima’ wa
fikra za chama kimoja, kwa sababu anazozijua mwenyewe amesahau au
ameshindwa au amefanya makusudi kwa sababu anazozjijua mwenyewe, kunukuu
kifungu cha 4(1) (e) cha maadili ya vyama vya siasa za mwaka 2007,
ambacho kinatoa haki kwa vyama vya siasa kuendesha shughuli zao za
kisiasa ikiwemo mikutano ya hadhara na maandamano kwa mujibu wa sheria.
Tulidhani kuwa Ofisi ya Msajili wa Vyama
vya Siasa ambaye si tu kwamba ni mlezi wa vyama vyote bali pia
anasimama kama mwamuzi wa mchezo wa mpira uwanjani, katikati ya timu
mbili uwanjani, angelisimamia kifungu hicho muhimu na kukitumia
kuwakemea na kuwaonya watawala, akiwemo Rais, Waziri Mkuu na Jeshi la
Polisi wasivunje sheria za nchi kuzuia shughuli za siasa nchini kwa
sababu yoyote ile kwa sababu hawako juu ya sheria za nchi hii.
Aidha, sasa tunaanza kushtuka na kuanza
kujiuliza maswali mengi kuhusu kasi ya Msajili wa Vyama vya Siasa
kujijengea utaratibu usiokuwa na kawaida kwa nafasi yake ya kisiasa na
kisheria, kuwa na kasi ya ajabu kutoa kauli au matamko yanayoonesha
kuwatetea/kuwalinda watawala wanapovunja sheria zinazosimamia vyama vya
siasa.
Jaji Mutungi amekuwa mahiri wa kuvikemea au hata kuvionya vyama vingine tofauti na CCM, kila vinapodai haki za kisiasa ambazo ziko na zinapaswa kutekelezwa kwa mujibu wa sheria, wala si kwa hisani ya mtu yeyote.
Jaji Mutungi amekuwa mahiri wa kuvikemea au hata kuvionya vyama vingine tofauti na CCM, kila vinapodai haki za kisiasa ambazo ziko na zinapaswa kutekelezwa kwa mujibu wa sheria, wala si kwa hisani ya mtu yeyote.
Waandishi wa habari na umma kwa ujumla
watakuwa mashahidi kwa namna ambavyo CCM wamekuwa wakitumia vyombo vya
dola, kuvikandamiza, kuvinyanyasa, kuviwekea mazingira magumu na
kuvinyima haki za kufanya siasa vyama vingine washindani wake kwa ajili
tu ya kulinda maslahi ya chama kilichoko madarakani.
Katika hali hiyo ambayo hata imekuwa
ikisababisha mauaji na umwagaji damu za watu wasiokuwa na hatia kwa
sababu tu ni wafuasi wa vyama vingine, Msajili wa Vyama vya Siasa
hajawahi kuthubutu kujitokeza hadharani kuwaonya na kuwakemea CCM na
walioko serikalini kuwa kutumia vyombo vya dola kwa manufaa yao ya
kisiasa ni kosa kwa mujibu wa sheria za nchi kupitia kifungu cha maadili
ya vyama vya siasa cha 5(1)(c), za mwaka 2007.
Tulitegemea kwa kutumia umahiri huo huo
wa kunukuu vifungu vya sheria na kanuni za maadili ya vyama vya siasa
ambao Msajili amekuwa akiuonesha dhidi ya vyama washindani wa CCM kila
vinapodai haki za msingi za kisiasa, angekuwa ameutumia pia kuwakemea,
kuwaonya au hata basi kuwakumbusha CCM na Rais Magufuli kwa kutumia
kifungu cha 5(1) (i) cha kanuni za maadili ya vyama vya siasa za Mwaka
2007, kuwa ni makosa kutumia mamlaka, rasilimali za serikali, vyombo vya
dola au wadhifa wa kiserikali, kuvikandamiza vyama vingine kwa manufaa
ya kisiasa ya upande mmoja.
Si hayo tu, Jaji Mutungi ama aliamua kuwa kimya au alikuwa na kigugumizi aliposikia;
- Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Rais John Magufuli na Jeshi la Polisi wakitoa kauli kinyume cha sheria wakitangaza na kuagiza kuzuia shughuli za kisiasa nchini kwa matakwa yao tu.
- Mabalozi na wanadiplomasia wakizuiwa kukutana na asasi zisizo za kiserikali au vyama vya siasa.
- Kukiukwa kwa misingi ya sheria, kanuni na taratibu za nchi katika uteuzi wa wakurugenzi na makatibu tawala.
- Hali tete inayoendelea Zanzibar baada ya watawala kuharibu uchaguzi mkuu mwaka jana kisha wakafanya uchaguzi wa marudio kwa maslahi ya CCM, kinyume kabisa na sheria za nchi.
Hayo ni baadhi tu ya masuala ya muhimu
ambayo ofisi ya msajili ilitarajiwa kuwa ingekuwa mstari wa mbele
kukemea na kuonya ili kuweka mizania ya ushindani wa kisiasa katika
usahihi wake.
Kwa mwenendo huu ambao usipoangaliwa na
kufanyiwa kazi ya kuurekebisha haraka, tunachelea kusema kuwa Ofisi ya
Msajili na Jaji Mutungi mwenyewe wataanza kujikosesha uhalali machoni pa
Watanzania ambao wasingependa kuona siasa ambayo ni maisha yao,
ikifananishwa kama vile ni jambo la kawaida tu lisilokuwa na maana.
Kupitia taarifa hii, tunamtaka Msajili
wa Vyama vya Siasa, Jaji Mutungi kuwa makini na utaratibu huo vinginevyo
Watanzania wataanza kuiweka ofisi yake na yeye mwenyewe kwenye kapu
moja na aliyekuwa mtangulizi wake, ambaye ilifika mahali wananchi
walimuona yeye binafsi, kupitia kauli zake, matendo yake na ofisi yake
kwa ujumla, sawa na sehemu ya chama kilichoko madarakani.
CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani nchini hakiwezi kuvumilia wala kukubali hiki kinachoanza kujionesha kuwa ni ‘double standards’ za
mtu anayetarajiwa kuwa mlezi na refarii, kujitokeza hadharani pale tu
ambapo maslahi ya chama tawala na watawala yanapoguswa lakini anakuwa
kimya na hata kuweka masikio nta mara vyama washindani wa CCM
vinapokandamizwa, kinyume kabisa cha sheria.
Kama chama chenye wanachama na viongozi
wanaojua haki na wajibu wao wa kikatiba na kisheria, tutaendelea kufanya
shughuli za kisiasa kwa namna itakayosimamia haki na matumaini ya
wananchi kwa ajili ya amani na utulivu wa kweli, kwa kuzingatia sheria,
kanuni na taratibu za nchi si kwa kufuata matamko, kauli au maelekezo ya
mtu yeyote.
Ni kwa kuzingatia dhana hiyo, maana
Kamati Kuu katika kikao cha dharura kilichofanyika mwishoni mwa juma
lililopita na maazimio yake kutangazwa juzi Jumatano, moja ya maazimio
yake ni kuanzisha operesheni ya UKUTA (Umoja wa Kupinga Udikteta
Tanzania) ambayo inalenga kuwaunganisha Watanzania wote bila kujali
tofauti zao zozote zile, kudai haki na matumaini dhidi ya udkiteta
katika nchi yao na kuzuia harakati za watawala kuataka kupora mamlaka ya
wananchi na kujiweka juu ya sheria kwa namna ile ile ambayo madikteta
hufanya.
Imetolewa leo Ijumaa Julai 29, 2016 na;
Prof. Mwesiga Baregu
Mjumbe wa Kamati Kamati Kuu
#MICHEZO>>>>Vitu alivyoongea bilionea Mohammed Dewji katika mpango wake wa kuinunua Timu Ya Simba.Fahamu zaidi hapa.
Kuelekea
mkutano mkuu wa Simba unaotaraji kufanyika Jumapili ya Julai, 31,
shabiki na mkeleketwa wa Simba ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa
Makampuni ya Mohammed Enterprises (MeTL Group), Mohammed Dewji
amezungumza mipango yake aliyopanga kuifanyia Simba kama akipata nafasi
ya kununua hisa asilimia 51 za klabu hiyo.
MO
amesema kuwa mipango yake ni kuwekeza Bilioni 20 na amepanga bajeti ya
klabu hiyo kwa mwaka iwe Bilioni 5.5, kiasi ambacho anaamini kuwa
kitaweza kubadili mwelekeo wa Simba kutoka ilivyo sasa na kurudisha zama
zake za kutwaa mataji ya ndani na kufika hatua nzuri kimataifa.
MO
alisema amefikia uamuzi wa kutaka kununua hisa katika klabu ya Simba
kutokana na mapenzi aliyonayo katika klabu hiyo na hana nia yoyote ya
kiabiashara na klabu hiyo kwani tayari ana biashara anazofanya ambazo
zinamuingizia pesa nyingi hivyo jambo hilo ni kuona timu aliyo na
mapenzi nayo ikifanikiwa.
“Nipo
tayari kuwekeza Bilioni 20 kama watanipa nafasi lakini tukubaliane kuwa
hakuna mtu atagusa pesa hizo pesa, tutauza bondi na kwa kila mwaka
tutaingiza Bilioni 3.5 na tutatengeneza mapato ya Bilioni 2 kila mwaka
ukijumlisha ni Bilioni 5.5 ambayo itakuwa ni bajeti ya mwaka,
“Inaniuma
sana kuona klabu imekuja juzi tu leo inatuzidi mafanikio lakini kama
Yanga na Azam bajeti zao kwa mwaka ni Bilioni 2.5 hadi Bilioni 3, sisi
tukiwa na bajeti ya Bilioni 5.5 tutakuwa tumewazidi na tutaleta
wachezaji wazuri na kocha mzuri,” alisema na kuongeza.
“Dhamira
yangu sio kupata Simba kibiashara, mimi Mungu kanijalia nina pesa nina
biashara ziadi ya 100, tumeajiri wafanyakazi wanafika 28,000 , jambo
ninalolitaka Simba ni kuwekeza, tubadili mfumo, tushinde mataji na sio
Tanzania pekee shabaha yangu ni kushinda mataji ya Afrika”
Aidha
MO alisema kuwa kama akipata nafasi atazungumza na viongozi wa Simba
ili kila mwanachama wa klabu wa muda mrefu apatiwe hisa bure kutokana na
kazi kubwa ambayo wameifanya katika klabu hiyo.
“Nitazungumza
na viongozi wa klabu tuone jinsi ambavyo tunaweza kuwapa bure wanachama
wa klabu ambao wamekuwa na timu kwa muda mrefu, wameshatoka jasho sana
na Simba hivyo tutawapa hisa za timu bure,” alisema MO.
Hata
hivyo MO aliongeza kuwa yupo tayari kwa lolote kama katika mkutano mkuu
wa Jumapili watamnyima nafasi ya kuwekeza katika klabu ya Simba na
kueleza kuwa anachoamini kwa sasa Simba haiitaji mdhamini bali Simba
inahitaji mwekezaji.
“Mimi
wakininyima kwa moyo mweupe kabisa sina tatizo na hili jambo hata
likifanikiwa halitakamilika kesho linaweza kuchukua muda sababu kuna
mambo ya kufanyiwa marekebisho na kusaini mikataba ila kama nikiona
mambo yanakwenda sawa kwa hicho kipindi nitaangalia jinsi gani
nitaisaidia Simba sababu nina mapenzi nayo,” aliongeza MO.
#YALIYOJIRI>>>>Lowassa Akoleza Moto CCM....Awata Wanaomuunga Mkono Ndani ya CCM Waendelee Kumpa Siri za Serikali.Fahamu zaidi hapa.
Aliyekuwa
mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa ana
uhakika kuwa bado kuna wanachama wanaomuunga mkono ndani ya CCM na sasa
anawataka waendelee kushikamana naye, kauli ambayo inaweza kuchochea
moto ndani ya CCM.
Katika
taarifa yake fupi kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana, Lowassa
amewahakikishia wananchi kuwa kwa sasa ana “ari, nguvu na hamasa kuliko
wakati mwingine wowote”.
Lowassa,
ambaye alikuwa waziri mkuu wa kwanza wa Serikali ya Awamu ya Nne,
alijiondoa kwenye chama tawala Julai 28 mwaka jana baada ya jina lake
kuondolewa kwenye orodha ya wagombea urais kwa tiketi ya CCM.
Kuondoka
kwake kulisababisha mawaziri wa zamani, wabunge, wenyeviti wa mikoa,
madiwani na wanachama wengine wa CCM, wakiongozwa na waziri mwingine
mkuu wa zamani, Frederick Sumaye kukihama chama hicho, hali
iliyosababisha ushindani kuwa mkubwa kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita, huku
CCM ikilalamikia kusalitiwa.
Wakati
CCM ikifikiria hatua za kuchukua dhidi ya wasaliti wa chama
wanaotuhumiwa kuunga mkono harakati za upinzani wakati wa Uchaguzi Mkuu
uliopita, Lowassa ameongeza petroli kwenye moto ulioanza kuwaka.
“Kwa wale wenzangu waliobaki CCM na wanaoniunga mkono, tuendelee kushikamana na kunipatia taarifa kwa hatima ya nchi yetu,” amesema Lowassa ambaye kwa sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.
“Nawashukuru Watanzania kwa kuendelea kuniunga mkono mimi na wenzangu ndani Chadema.”
Kauli
hiyo kuwa kuna watu ndani ya CCM ambao wanampatia taarifa mbunge huyo
wa zamani wa Monduli na ombi lake la kutaka waendelee kumpa taarifa,
inaweza kusababisha hali ngumu zaidi kwa chama hicho, ambacho kinaamini
kuwa makada wake walikihujumu wakati wa uchaguzi kwa kumfanyia kampeni
kisiri.
Katika uchaguzi huo, Rais John Magufuli alishinda kwa kupata asilimia ndogo ya kura kulinganisha na watangulizi wake.
Ingawa
alipata kura milioni 8.8 na Lowassa kufuatia kwa kupata kura milioni
6.07, ushindi huo ni wa asilimia 58.46 dhidi ya asilimia 39.67
kulinganisha na ushindi wa asilimia 61.17 aliopata Kikwete mwaka 2010
dhidi ya asilimia 26.34 alizopata Dk Willibrod Slaa wa Chadema.
Tangu
Januari mwaka huu, CCM imekuwa ikijadili wasaliti hao katika ngazi ya
wilaya na taarifa za mapendekezo ya hatua dhidi yao kutumwa Halmashauri
Kuu kwa ajili ya uamuzi wa mwisho.
Katika
hotuba yake ya kuaga, Jakaya Kikwete alimkabidhi mwenyekiti mpya wa
CCM, Rais Magufuli ripoti ya hali ilivyokuwa kwenye uchaguzi, akisema
yeye ndiye atakayeamua adhabu dhidi ya wale wote walioonekana kufanya
makosa. CCM imeshasema kuwa wasaliti wote ni lazima washughulikiwe.
Katika taarifa yake ya jana, Lowassa ameeleza kuwa uamuzi alioufanya wa kuihama CCM na kujiunga na Chadema “haukuwa
rahisi, lakini kwa ushupavu, ujasiri na mwongozo wa Mungu nilifanya
hivyo” na kwamba huo ni “uamuzi wa kihistoria katika nchi yetu.
“Najivunia
kwa uamuzi ule, kwani umewafungua macho Watanzania wengi na kuimarisha
demokrasia. Nimeingia Chadema nimewakuta viongozi na wanachama walio na
moyo wa dhati wa kuliletea maendeleo Taifa lao kivitendo,” anasema Lowassa katika taarifa yake fupi.
“Watanzania
bado wanataka mabadiliko na imezidi kuthibitisha kuwa hawawezi kuyapata
ndani ya CCM. Watanzania wanataka sera na mtu mbadala wa kuongoza
mabadiliko hayo. Vyote hivyo watavipata ndani ya Chadema na Ukawa kwa
jumla.”
#YALIYOJIRI>>>>Pacha wa Magufuli Azua taharuki kariakoo.Fahamu zaidi hapa.
Mtu mmoja ambaye hajafahamika jina lake amezua taharuki mitaa ya
k,koo baada ya kuwa na muonekano unaofanana na Rais wa jamuhuri ya
muungano wa Tanzania Jonh Pombe Magufuli.
Mtu huyo ambaye anafanana sana na Rais Magufuli alionekana kufatwa kila anapoenda huku watu wakiwa wamemzunguka wakidhani Rais Magufuli Kavamia Soko la K,koo..
Mtu huyo ambaye anafanana sana na Rais Magufuli alionekana kufatwa kila anapoenda huku watu wakiwa wamemzunguka wakidhani Rais Magufuli Kavamia Soko la K,koo..
#YALIYOJIRI>>>Mwanamuziki Koffi Olomide aachiwa huru kutoka jela baada ya kutumikia kifungo kwa siku 2.Fahamu zaidi hapa.
Koffi
Olomide Alikamatwa Jumanne July 26 2016 nyumbani kwake Kinshasa kwa
tuhuma za kumshambulia dancer wake wa kike wakati wakiwa uwanja wa ndege
wa kimataifa wa Jomo Kenyata Nairobi na baadaye ikawa imeripotiwa kuwa
amehukumiwa kwenda jela miezi 18 na adhabu hiyo kutajwa kuwa haitakuwa
na faini.
Taarifa
zilizoripotiwa ni kwamba Koffi Olomide kaachiwa huru baada ya kutumikia
kifungo cha siku mbili kati ya miezi 18 aliyohukumiwa awali.
BBC
imeripoti kuwa kuachiwa kwa koffi Olomide kumekuja baada ya Mahakama ya
Kinshasa kusema kuwa hawakuona sababu za kutosha za kuhukumiwa kwa
Koffi Olomide kutokana na tukio alilofanya JKIA.
Pamoja
na baadhi ya vyombo vya habari Afrika kuripoti kwamba Koffi alihukumiwa
kifungo cha miezi 18 jela , Promoter wake wa nchini Kenya Jules Nsana
amekanusha madai hayo na kusema kesi dhidi ya Koffi ilikuwa bado iko
kwenye uchunguzi na kwamba baada ya uchunguzi wamebaini hakuna ushahidi
wa kutosha wa kumtia hatiani Koffi Olomide.
Promoter Jules amesema Olomide alimpigia simu akamtaka aombe msamaha kwa wakenya wote kwa niaba yake.



























