Serikali
kupitia Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira NEMC
limekitoza faini ya shilingi milioni 15, Kiwanda maarufu cha kutengeneza
simenti cha Dagonte Industry limited kilichopo mjini Mtwara kusini
mwa Tanzania, kwa kosa la kukiuka sheria ya mazingira ya mwaka 2004 na
kanuni zake.
Katika
siku ya Pili ya Ziara ya ziara ya Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu
wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Luhaga Mpina Mkoani Mtwara Imebainika
kuwa kiwanda hicho cha Dangote chenye muda wa miezi mitatu tangu kianze
kazi ya kutengenza siment, kimefanya uchafuzi wa mazingira kwa kukosa
sehemu maalum ya kuhifadhi taka katika kiwanda hicho, kutokuwa na
utaratibu mzuri wa kuhifadhi taka zitokanazo na makaa ya mawe kiwandani
hapo, kukosa vyoo kwa ajili ya matumizi ya wateja wao ambao ni madereva
na makondakta wanao chukua mzigo wa siment kiwandani hapo, na
kusafirisha kwenda sehemu mbali mbali za nchi, pamoja na kutokusakafia
sehemu ya nje ya kiwanda hicho ambapo imeelezwa kuwa eneo hilo la nje
wakati wa kipindi cha mvua mazingira yake huatarisha afya ya watumiaji
wa eneo hilo.
Kwa
Mujibu wa Naibu waziri Mpina, adhabu hiyo kwa kiwanda cha Dangote
inayotakiwa kulipwa ndani ya wiki mbili, inaenda sambamba na
urekebishaji wa kasoro hizo kiwandani hapo pamoja na kuhamsha uongozi wa
kiwanda hicho kwa kudharau sheria ya mazingira, na kutaka kiwanda hicho
kuajiri afisa mazingira ataeshughulia changamoto hizo.
Kwa
upande wake Meneja utumishi na utawala wa kiwanda hicho Bw. James
Kajeli aliomba serikali kusamehe adhabu hiyo kwani kiwanda kilikuwa
kwenye mpango wa kufanya marekebisho hayo na kuongeza kuwa kutokufanya
hivyo kwa wakati ni kujisahau kwa kibinadamu, na kuwa utengenezaji wa
baadhi ya miundombimu kiwandani hapo ulicheleweshwa na upatikani wa
baadhi ya vibali kutoka katika taasisi za serikali na si kudharau sheria
ya mazingira.
Naibu
waziri Mpina Pia alitembelea kiwanda cha kutengeneza gas cha Madiba na
kukisifu kwa utekelezaji wa sheria za mazingira na kuviasa viwanda vya
serikali, kuwa mfano katika kutii sheria za mazingira.
Ziara
ya Mhe. Mpina pia ilihusisha ukaguzi wa kiwanda cha kubangua korosho
cha micro mix cha mjini Mtwara, kiwanda cha gas cha Solvochemi pamoja na
fukwe ya mnazi bay iliyoathiriwa na athari zitokanazo na mabadiliko ya
tabia nchi.
0 comments:
Post a Comment