ZITTO Kabwe na Maalim Seif Sharif Hamad kwa pamoja wameitwa jijini Philadelphia, Marekani.
Maalim Seif ni Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) ambapo Zitto ni Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo.
Wanasiasa
hao wameitwa kuhudhuria mkutano mkuu wa Chama cha Demokratiki
utakaomthibitisha Hillary Clinton kuwa mgombea urais wa Marekani kupitia
chama hicho.
Marekani
inatarajia kufanya Uchaguzi Mkuu tarehe 8 Novemba mwaka huu ambapo
Clinton atathibitishwa kwenye mkutano huo kupambana na Donald Trump wa
Chama cha Republican.
Maalim Seif na Zitto ndio wanasiasa pekee nchini waliopata mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.
Abdallah
Khamis, Ofisa Habari wa ACT- Wazalendo amesema wakati Zitto akiwa
kwenye mkutano huo, atapata fursa ya kufanya mazungumzo na viongozi
mbalimbali wa kisiasa duniani.
Taarifa zinaeleza kuwa, viongozi hao ni wawakilishi wa wanasiasa mahiri kutoka upinzani nchini Tanzania.
0 comments:
Post a Comment