Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jana kimefungua rasmi kesi dhidi ya Serikali katika mahakama ya Afrika Mashariki kupinga zuio la kufanya mikutano ya hadhara ya kisiasa.
Naibu
Katibu Mkuu wa Chadema (Bara), John Mnyika aliwaambia waandishi wa
habari kuwa wameamua kufungua kesi hiyo kwakuwa tamko hilo la Serikali
ni kinyume cha katiba na mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja
na sheria ya vyama vya siasa.
Mnyika
ambaye aliambatana na mwanasheria wa chama hicho, John Mallya alisema
kuwa wamekusanya ushahidi wa kutosha wa matamko ya katazo la kufanyika
mikutano ya kisiasa na namna chama hicho kilivyozuiwa kufanya mikutano
hiyo sehemu mbalimbali nchini.
“Tumeleta
vielelezo vya zuio lenyewe la polisi kama ushahidi wa kwamba ni kweli
polisi wa Tanzania wametoa agizo kama hilo. Pili, tumeleta vielelezo vya
mikutano iliyozuiwa… mikutano ya Kahama, Mahafali ya wanachuo wa
Chadema kule Dodoma, Mahafali yaliyofanyika kule Moshi na mikutano
mingine,” alisema Mnyika.
“Katiba
na sheria zetu zingekuwa zinaruhusu kumburuza moja kwa moja mahakamani
Rais Magufuli, basi leo mashtaka yangekuwa dhidi ya Magufuli. Lakini
mwanasheria wa Serikali anasimama kwa niaba ya Serikali,” aliongeza.
Naibu
Katibu Mkuu huyo wa Chadema alisema kuwa mbali na Mwanasheria Mkuu wa
Serikali, Wamemshtaki pia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
kwani analo jukumu la kusimamia mikataba ya Jumuiya hiyo.
0 comments:
Post a Comment