Serikali
imetakiwa kufanya marekebisho ya sheria mbalimbali ambazo zimeonekana
kuwa kandamizi ikiwepo ile sheria za vyombo vya habari ambazo
zinakandamiza uhuru wa vyombo vya habari pamoja na waandishi wenyewe.
Akitoa
ripoti ya nusu mwaka mbele ya wanahabari kuhusu hali ya haki za
binadamu nchini Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Bi
Hellen Kijo Bisimba amesema kuwa vyombo vya habari havifanyi kazi kwa
uhuru kwani zipo sheria ambazo bado ni kandamizi.
”Vyombo
vya habari bado havina uhuru kwani sheria kandamizi bado zinatumika
mfano, gazeti la mawio kufungiwa na kutakiwa kutoandika nakala zake hata
kwenye mitandao bila sababu maalumu”.Ilielezwa katika ripoti ya kituo hicho
Aidha
ripoti hiyo ya miezi sita imesema kuwa wananchi bado wananyimwa haki
zao za msingi ikiwa ni pamoja na kunyimwa haki ya habari kwasababu
serikali imeamua kutorusha matangazo ya bunge kwa sababu mbalimbali
ambazo zinakinzana.
Katika
ripoti hiyo pia imegusa haki za kujumuika ambapo kituo hicho kimesema
matamko ya jeshi la polisi hasa katika kuzuia mikutano ya vyama
imeonekana kupendelea chama tawala huku vyama vya upinzani vikiwa
vinakandamizwa.
”Mfano
mkutano wa Chadema shinyanga ulipewa vibali vyote lakini baadae ukaja
kutawanyishwa kwa kutumia nguvu mpaka mabomu, aidha ACT walikuwa na
kongamano la kuchambua bajeti lakini jeshi la polisi walizuia lakini
wakati huo huo CCM walikubaliwa kufanya mkusanyiko” Ilieleza semu ya ripoti ya Kijo Bisimba.
Pamoja
na hayo ripoti hiyo imetoa mapendekezo kwa Serikali ikiwa kuboresha
sheria hizo kandamizi kwa wananchi pamoja na kuachia vyombo vya habari
kufanya kazi zake pasipo kuingiliwa sambamba na Vyama vya siasa kupewa
haki sawa.
0 comments:
Post a Comment