Kiongozi
wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amepata ajali ya kuanguka
ghafla alipokuwa akitembea kuelekea kwenye jukwaa lililoandaliwa kwa
ajili ya kuendesha ibada, Czestochowa nchini Poland.
Papa
Francis mwenye umri wa miaka 79 alisaidiwa kwa haraka na wasaidizi wake
na kufanikiwa kuamka na kuendelea na safari hadi kwenye kiti
kilichoandaliwa.
Kwa
bahati nzuri, kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki alionekana kuwa katika
hali yake ya kawaida ambapo aliendelea kuongoza ibada hiyo iliyokuwa
ikirushwa moja kwa moja kupitia vituo mbalimbali vya runinga na
kuangaliwa na mamilioni ya watu.
Kwa
mujibu wa Daily Mail, Papa Francis anasumbuliwa na ugonjwa unaojulikana
kama Sciatica, ugonjwa ambao wakati mwingine hushusha maumivu ya ghafla
kwenye miguu kutoka mgongoni.
0 comments:
Post a Comment