Tuesday 19 July 2016

#MICHEZO>>>>USAJIRI UINGEREZA KUHUSU POGBA KUTUA OLD TRAFFORD.Fahamu zaidi hapa.

Paul Pogba anatua Manchester United
Siku nyingine tena Paul Pogba yuko kwenye kurasa za mbele za magazeti ya Ulaya.

Gazeti la La Gazzetta dello Sport la nchini Italy limeandika habari ambayo huenda ikawakosha mashabiki wa Manchester United kuhusu kiungo huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye miaka 23 kurejea kwenye himaya ya Old Trafford

Kichwa cha habari cha gazeti hilo kinaashiria kwamba Juventus wanamuuza Pogba kwenda United huku wakifanya mipango ya kumnasa mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain kutua Turin.

Habari mpya kuhusu dili la Pogba kutua United
Ukisoma habari hiyo kwa undani inasisitiza kwamba, wakala wa Pogba Mino Raiola ameshasafiri kwenda England kusikiliza ofa ya Man United juu ya mteja wake.

Ofa kutoka Old Trafford ni euro milioni 100 huku kukitarajiwa kuwa na nyongeza ya euro 24 nyingine.

Ongezeko hilo la euro milioni 24 halijawekwa wazi ni kwa ajili ya nini, lakini inawezekana wanaweza kuweka kipengele cha kuongezewa mkwanja iwapo Pogba ataisaidia United kushinda taji la Champions League au kama atafanikiwa kutwaa Ballon d’Or.

Pogba anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano kuitumikia United ambapo atavuna kitita cha euro milioni 12 kwa msimu kutokana na mshahara.

0 comments:

Post a Comment