MATAJIRI wa Ligi Kuu Bara, Azam wanatarajia kuingia msimu mpya wakiwa wamegusa; benchi la ufundi na safu ya ushambuliaji na tayari imetangaza kuachana na Kipre Tchetche aliyejificha jijini Dar es Salaam.
Azam imefanya mabadiliko makubwa katika benchi la ufundi, imeleta makocha Wahispaniola; Kocha Mkuu Zeben Hernandez, msaidizi Yeray Romero, kocha wa viungo, Jonas Garcia na wa makipa, Pablo Borges.
Makamu Mwenyekiti Azam, Nassoro Idrissa ‘Father’ alisema: “Nadhani mabadiliko makubwa yapo benchi la ufundi na safu ya ushambuliaji, tunatafuta mbadala wa Allan Wanga na Kipre Tchetche, nafasi za wachezaji wa kigeni zipo nne; Wanga, Racine Diouf na Kavumbagu waliondoka, Kipre tupo hatua za mwisho kukamilisha uhamisho wa kwenda Oman,” alisema.
Azam ina nyota wanne wageniwanaofanya majaribio kutoka Niger, Zimbabwe na Ivory Coast.
0 comments:
Post a Comment