Katika
kuhakikisha wanaziba nafasi ya mshambuliaji wao, Kipre Tchetche
anayeusumbua uongozi wa Klabu ya Azam FC, mtendaji mkuu wa klabu hiyo,
Saad Kawemba yupo nchini Ghana kumalizana na straika hatari wa timu ya
Medeama FC, Kwame Boahene.
Licha
ya Azam kujaza utitiri wa wachezaji wa kigeni ambao wanafanya majaribio
ndani ya timu hiyo kwa sasa wakiwemo washambuliaji watatu, Mniger,
Morsi Mussa Issa, Mzimbabwe, Bruce Kangwa na Ibrahima Fofana raia wa
Ivory Coast.
Lakini
wakaona ni bora kwenda kusaka straika mwingine kwa ajili ya kuziba
pengo la Tchetche ambaye anadaiwa kuwa kwenye mazungumzo na moja ya timu
za Oman.
Azam
walianza kumfuatilia mshambuliaji huyo wakati Medeama ilipocheza na
Yanga hapa nchini kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya
makundi, ambapo bosi huyo alifanikiwa kuzungumza na viongozi wa Medeama
kabla ya kwenda kumuangalia tena katika mchezo wa marudiano dhidi ya
Yanga uliopigwa jana Jumanne huko Ghana.
Taaarifa
za uhakika kutoka ndani ya timu hiyo, zinasema kuwa bosi huyo licha ya
kumuangalia uwezo wake kwenye mchezo huo, lakini pia alipata nafasi ya
kumshuhudia katika mazoezi ya mwisho yaliofanyika juzi Jumanne kabla ya
mchezo huo wa jana na Yanga.
Ofisa
habari wa Azam FC, Jaffar Idd, amelithibitishia Championi Jumatano
kuwa, Kawemba yupo nchini Ghana kwa ajili ya kumuangalia mchezaji huyo
na wengine ili kuziba nafasi zenye upungufu.
“Ni
kweli Kawemba yupo Ghana na amekwenda kuwaangalia wachezaji ambao kama
mambo yakienda vizuri basi atarudi nao kwa ajili ya kuitumikia timu
yetu, lakini pia akitoka huko atakwenda Ivory Coast kuangalia wachezaji
wengine,” alisema Idd.
0 comments:
Post a Comment