MAOFISA
 Ugavi wanne wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Kitengo cha Maafa), wamepandishwa 
kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam  kwa 
madai ya kuiba mali za ofisi hiyo zenye thamani ya Sh milioni 100.
Wakisomewa
 hati ya mashtaka mbele ya Hakimu, Respicius Mwijage, Wakili wa 
Serikali, Jackson Chidunda aliwataja washtakiwa hao, kuwa ni Ahmed 
Yusuph(48) Ofisa ugavi, Martine Tyeah(31) Ofisa Ugavi Msaidizi, Mwahija 
Kimata(55),Ofisa ugavi msaidizi na Halima Mwanjiro(33) Ofisa Ugavi.
Alidai 
 washtakiwa hao, wanadaiwa kati ya Aprili, 2014  na Septemba, mwaka huo 
huo katika eneo la Keko lililopo karibu na Ofisi ya Bohari Kuu ya 
Madawa(MSD), Temeke jijini Dar es Salaam, wakiwa waajiriwa wa Ofisi ya 
Waziri Mkuu, wanadaiwa  kuiba mabati 5074,Sufuria 200 na mikeka 348 
vyenye thamani ya Sh 100,164,000.
Alidai 
 mali hizo zinamilikiwana Ofisi ya Waziri Mkuu Kitengo cha Maafa  ambazo
 zilitolewa kwa ajili ya maafa kupitia kitengo hicho, lakini washtakiwa 
hao wanadaiwa kuchukua kinyume cha sheria.
Alidai upelelezi wa shauri hilo,bado haujakamilika na kuiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hata
 hivyo, Hakimu Mwijage aliwataka kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja 
ambaye atasaini bondi ya Sh milioni 25 ambapo washtakiwa hao walikidhi 
mashart hayo na kuachiliwa kwa dhamana.
Shauri hilo, limeahirishwa hadi Agosti 22, litakapotajwa tena.
Wakati
 huo huo, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imempandisha kizimbani raia wa
 China, Senxin Van baada ya kubainika kufanya kazi kinyume na kibali 
chake.
Akisomewa
 hati ya mashtaka mbele ya Hakimu Huruma Shahidi, Wakili wa Serikali, 
Novatus Mlay alidai mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo mnamo Julai, 12, 
mwaka huu katika kampuni ya uwekezaji ya Tenglong iliyopo Kinondoni 
jijini Dar es Salaam ambapo aliajiriwa kama daktari wakati kibali chake 
kinamruhusu kufanya kazi katika kampuni ya kutengeneza viatu ya Tong 
Xing kama Mkurugenzi.
Katika utetezi wake, mshtakiwa huyo aliiomba mahakama hiyo kumsamehe kwa sababu ni babu mwenye wajukuu na mlezi wa familia na kwamba katika kampuni hiyo ni Mkurugenzi ambaye  ameajiri watanzania wengi.
 








 




 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
0 comments:
Post a Comment