Tume
ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imewatoa hofu wanafunzi waliohitimu katika
vyuo vilivyozuiwa hivi karibuni kufanya udahili, huku ikikanusha
taarifa za kuzifungia udahili wa kozi tofauti vyuo 22 zilizozagaa juzi.
Hivi
karibuni TCU ilitangaza kusimamisha kufanya udahili vyuo vitano baadhi
vikiwamo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Francis
cha Ifakara Morogoro, Chuo cha Mtakatifu Joseph cha Dar es Salaam na
Chuo cha IMTU cha Dar es Salaam vyote kwa kozi ya udaktari.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi jana, Kaimu Katibu Mtendaji wa TCU,
Eliuther Mwageni alisema kufungiwa kwa vyuo hivyo ni kwa muda mpaka
vitakapokabidhi vigezo vinavyotakiwa.
"Kuna
vigezo vinavyotakiwa kufikiwa ili chuo kiweze kusajiliwa na hivi vyuo
hatujavifungia ila tumevisimamisha kwa muda mpaka vikidhi vigezo vyetu.
0 comments:
Post a Comment