Wednesday, 2 March 2016

BREAKING NEWS>>>>Jiji la Mwanza Lalipuka kwa shangwe...Wenje Ashinda Kesi ya Pingamizi Lililowekwa na Mabula Mahakamani.Fahamu zaidi hapa.

Aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana Ezekiah Wenje ameshinda pingamizi aliyowekewa na mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula
Kesi ya msingi itaanza kusilizwa tarehe 6|03|2016.
Jiji limesimama kwa muda watu wanashangili kwa furaha mama ntilie machinga wanashingilia taarifa kamili tutawaletea baadae endelea kufatilia hii page ya Blog: hebronmalele.blogspot.com

#YALIYOJIRI>>> Rais Magufuli akutana na kufanya Mazungumzo na Rais Kenyatta na Rais Kagame.Fahamu zaidi hapa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais wa Kenya Uhuru Kenyata kabla ya kuanza kwa mkutano wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.PICHA NA IKULU.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, kando ya Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki unaofanyika Mkoani Arusha, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuimarisha mahusiano hususani katika masuala ya kiuchumi.

Baadhi ya maeneo waliyokubaliana kutilia mkazo katika mahusiano hayo, ni pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo inayounganisha nchi mbili ikiwemo ujenzi wa miundombinu, kukuza biashara na kuzalisha ajira kupitia viwanda.Rais Uhuru Kenyatta amesema amefurahishwa sana kuona Rais Magufuli yupo tayari kuhakikisha nchi ya Kenya na Tanzania zinakuwa karibu, na miradi ya maendeleo inaharakishwa.

"Kwa sababu nia yetu sisi ni kuona maendeleo ambayo yatagusa mwananchi wa kawaida, tumalize umasikini, uchumi ukue, na hivyo hatuwezi kufanya tukiwa tumetengana" Amesisitiza Rais Kenyatta.

Kwa upande wake Rais John Pombe Magufuli, amesema Tanzania na Kenya zina kila sababu ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara hasa katika ujenzi wa viwanda utakaozalisha ajira kwa kuwa watu wake ni wamoja.

"Wazee wetu Mzee Kenyatta na Mzee Nyerere walijenga mazingira mazuri ya kuwa na nchi hizi mbili wakati wakipigania uhuru, sasa sisi vijana wao ni wakati wetu kwenda mbele kwa ajili ya maendeleo" amebainisha Rais Magufuli.Dkt. Magufuli amebainisha kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki zinajenga mahusiano na ushirikiano zinalenga kupata manufaa hayo ya kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wake.

Ameutaja mradi mmojawapo kuwa ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka Tanzania kwenda nchini Kenya kupitia Namanga, na akaongeza kuwa Tanzania itakapoongeza uzalishaji wa umeme na kuanza kuvuna gesi, itaiuzia pia Kenya, halikadhalika Kenya nayo itauza bidhaa zake Tanzania.

Kabla ya kukutana na Rais Kenyatta, Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame, ambapo viongozi hao wamekubaliana kuzidisha mahusiano kati ya Tanzania na Rwanda ambapo Rais Magufuli amemhakikishia kuwa serikali yake itakamilisha ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani "Standard Gauge" ili kurahisha usafirishaji wa bidhaa na watu.

Rais Kagame amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake bora uliolenga kuimarisha uchumi, ikiwemo kuimarisha bandari ya Dar es salaam ambayo Rwanda inaitegemea na ujenzi wa Reli ya Kati ambayo pia ni tegemeo kubwa kwa uchumi wa Rwanda.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiano, IKULU
Arusha
02 Machi, 2016

Tuesday, 1 March 2016

#YALIYOJIRI>>> WAZAZI WALALAMIKA KUFUNGWA KWA MATAWI YA CHUO KIKUU CHA ST, JOSEPH.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

BAADHI   ya wazazi wa wanafaunzi waliokuwa wakisoma Chuo Kikuu cha St Joseph katika  matawi ya Arusha na Songea wametupa lawama kwa Tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) kwa hatua yake ya kufuta vibali vya kuanzisha matawi hayo na kwamba hali hiyo imewathiri watoto wao.

February 26 mwaka huu ,tume ya vyuo vikuu ilitangaza kufuta kibali cha chuo kikuu cha St Joseph (SJUIT) tawi la Arusha ikiwa ni wiki moja imepita tangu kuchukuliwa kwa hatua kama hiyo kwa Chuo kikuu cha St Joseph tawi la Songea,vyuo vilivyoko chini ya shirika la kitawa la Dada wa Maria Imakulata (DMI).

Wakizungumza na mtandao huu kwa nyakati tofauti baadhi ya wazazi wameeleza kusikitishwa na hatua hiyo huku wakidai kuwaathili kisaikolijia watoto wao ambao wengine walikuwa katika maandalizi ya mitihani.

“Nadhani ingekuwa ni jambo la busara  kwa TCU kukaa meza ya mazungumzo na uongozi wa chuo badala ya kuchukua hatua ya kukifutia vibali….Chuo hiki kimekuwa kikitoa mchango mkubwa katika kuzalisha wataalumu mbali mbali.”alisema Mrisho Sume.

Nchi yetu ina wataalamu wachache  katika sekta ya Sayansi na Teknalojia ,chuo hiki kilikuwa ni kimojawapo kinachotoa wataalamu hao hivyo mchango wake unapaswa kuheshimika na kusaidiwa pale inapobidi,” aliongeza Sume ambaye mwanaye alikuwa akisoma katika chuo cha Sayansi ya kilimo katika chuo hicho tawi la Songea.

Mzazi mwingine alijitambulisha kama Mariam Ali alisema taarifa alizokuwa nazo ni kuwa uamuzi wa kufunga baadhi ya matawi hayo ulifikiwa bila ya kukipa taarifa chuo hicho juu ya mapungufu yaliyopo ikiwa ni pamoja na kukipa muda wa kuyafanyia kazi.

“Binti yangu alikuwa akisoma tawi la Arusha na nimepata taarifa kuwa  timu ya ukaguzi kutoka tume ilifika chuoni hapo   kwa ajili ya ukaguzi lakini cha kushangaza ni kuwa chuo hakikupewa taarifa ya mapungufu yaliyoonekana ili yafanyiwe kazi na badala yake kililetewa barua za kufutiwa vibali.”alisema Mariam.

Uamuzi ulifanywa ni wazi haukuzingatia haki na unatuumiza sisi wazazi pamoja na watoto wetu, tulitegemea TCU kukipatia chuo  ripoti ya mapungufu waliyoyagundua na kupewa muda wa kuyafanyia kazi  na endapo kingeshindwa kuyafanyia kazi katika muda ambao kimepewa tume ingekuwa na haki ya kutoa adhabu,” aliongeza Mariam.

Naye John Budigle alisema tangazo lilitolewa na TCU kuhusu kufunga vyuo hivyo lilisema moja ya matatizo yaliyopelekea kufungwa ni migomo ya wanafunzi huku akiongeza kuwa migomo yote  ilitokana na kucheleweshewa mikopo na siyo matatizo ya chuo .

“Mimi kwa mtizamo wangu naona kama TCU imetumia nguvu kubwa kwenye suala hili, kama chuo kilifanya makosa kilipaswa kupewa maelekezo ya kushughulukia kasoro au mapungufu kwani hakuna chuo kisichokuwa na mapungufu hata hivyo vya umma. “alisema Budigle.

“Hatua hii inawavunja moyo wawekezaji katika sekta ya elimu. Hawa ni wadau katika elimu na ni vizuri TCU wakatuchukuliwa hivyo. Wao ni wasimamizi ambao wanatakiwa kuwaongoza na kuwarekebisha pale wanapokosea. Kitendo cha kukifutia vibali bila kufuata haki kinawavunja moyo wadau wa elimu pamoja na wanafunzi pia,” aliongeza Budigle.

Akitangaza hatua hiyo hivi karibuni  Katibu Mtendaji wa TCU, Profesa Yunus Mgaya, alizitaja sababu za kufikia uamuzi huo kuwa ni matukio ya migogoro ya muda mrefu baina ya uongozi wa chuo hicho na wanafunzi na ukiukwaji wa sheria za uendeshaji wake kama ulivyobainishwa na Sheria ya Vyuo Vikuu.

#YALIYOJIRI>>>Polisi ,UKAWA Ngoma Nzito,Naibu Katibu Mkuu CUF Nassor Ahmed Mazrui Naye Atakiwa 'Kujisalimisha' Polisi Kwa Mahojiano.Fahamu zaidi hapa.

Jeshi la Polisi limeendelea na kamatakamata ya wapinzani wa vyama vinavyounda Ukawa katika maeneo mbalimbali likieleza sababu tofauti za kijinai zinazohusishwa na masuala ya kisiasa.

Mpaka sasa wabunge wa upinzani waliokamatwa ni; Halima Mdee (Kawe), Mwita Waitara (Ukonga) na Peter Lijualikali (Kilombero), wote wa Chadema na baadhi ya madiwani wa chama hicho katika Jiji la Dar es Salaam.

Vilevile, imeelezwa kuwa Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea alikuwa anatafutwa kuunguanishwa na wenzake.

Pia, baadhi ya wanasiasa wa CUF Zanzibar wamekamatwa na kuhojiwa kwa madai ya kuwatusi viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ). 

Viongozi wa CUF waliohojiwa na polisi mpaka sasa ni Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Omar Ali Shehe na Kiongozi wa Mkakati wa Ushindi, Mohamed Sultan Mugheir ‘Eddy Riyami’ ambaye yuko nje kwa dhamana.  

Mbali na viongozi hao, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Nassor Ahmed Mazrui  jana  amepatiwa barua ya wito  na Polisi Zanzibar  ikielezwa kuna mambo yanamhusu.

Hii ni mara ya pili kwa Mazrui kuitwa polisi tangu kufutwa kwa uchaguzi wa Oktoba 25, huku CUF ikidai kuwa huo ni mwendelezo wa mkakati maalumu dhidi ya viongozi wa chama hicho.
Jana, Kaimu Mkurugenzi wa Habari na Uhusiano wa Umma wa CUF, Maalim Hamad Masoud Hamad alidai kuwa hatua hiyo ni utekelezaji wa maagizo ya kisiasa ya kutaka kumkamata kila kiongozi wa juu wa CUF kuelekea uchaguzi wa marudio.

“Kwa viongozi wa CUF hili halishangazi, nahisi ingelikuwa ni hatua ya kushangaza sana iwapo wanaoitwa kuhojiwa na polisi ni viongozi wa vyama vingine.

"Sisi upande wetu hili ni jambo la kawaida mno na watu wasishangae,” alisema.

Mazrui ambaye pia alikuwa Waziri wa Biashara na Uwekezaji, ametakiwa kuripoti Makao Makuu ya Polisi, Ofisi ya Upelelezi Ziwani mjini hapa kesho saa 2.00 asubuhi na kuonana na mkurugenzi wa makosa ya jinai Zanzibar.

Polisi Zanzibar imethibitisha kuwapo wito huo ikisema kuna mambo muhimu yanayomhusu mwanasiasa huyo.

#YALIYOJIRI>>> President Magufuli and President Museveni agree on building oil pipeline frona Tanga to Uganda.Fahamu zaidi hapa.

The President of the United Republic of Tanzania Dr. John Pombe Magufuli who is The current chairman of the East African Community (EAC) has held talks with His Excellency Yoweri Kaguta Museveni, The President of the Republic of Uganda in which among other things the two leaders have agreed to the construction of an oil pipeline from the port of Tanga in Tanzania to Uganda.

President Museveni paid a visit to President Magufuli at the state lodge in Arusha this evening soon after arriving in the country from Uganda to attend the 17th East African Community Heads of State Summit to be held at Ngurudoto Hotel in Arusha tommorow.

Speaking after private talks between the two leaders, President Magufuli said they have agreed to implement the Tanga-Uganda oil pipeline project for the benefit of both countries and other East African countries.

He said the oil pipeline will be 1,120 kilometers long and that the project will create more than 15,000 jobs.

President Magufuli added that, apart from constructing the oil pipeline, they also discussed increasing trade within the East African countries, building factories and creating jobs through various productive sectors.

Furthermore, President Magufuli said during the summit, Partner States will also discuss about South Sudan joining the East Africa Community (EAC).

He said that South Sudan becoming a member of the EAC means the region will be able to trade in an area with approximately 150 million people and therefore benefiting greatly.

On his part, President Yoweri Kaguta Museveni besides concurring with President Magufuli, has congratulated his Tanzanian counterpart on his leadership performance so far, and he has said that it is his hope that EAC Partner States will be in position to match President Magufuli’s speed in bringing development.

Gerson Msigwa
Ag. Director for Presidential Communications,
Arusha
1 March 2016

NEY WA MITEGO AJIBIWA NA KIMBUNGA NYIMBO YAKE YA "SHIKA ADABU YAKO" ISIKILIZE NA KUDOWNLOAD HAPA.

Hii ni nyimbo ambayo NEY WA MITEGO amejibiwa na KIMBUNGA baada ya kutoa nyimbo yake ya "MCHANE" isikilize hapa chini.

#YALIYOJIRI>>>Wauguzi sita Temeke wasimamishwa Kazi kwa kuuza gloves.Fahamu zaidi hapa.

Naibu Waziri wa Afya, Dk Hamis Kigwangalla amewasimamishwa kazi wauguzi sita katika hospitali  ya  Temeke kwa kosa la kuomba rushwa.

Wauguzi waliosimamishwa ni Hadija Salum, Beatrice Temba, Agnes Mwampashe, Elizabeth Mwilawa, Mariam Mohamed na Marion Said, ambao walikuwa zamu katika wodi ya wajawazito wakati wa tukio hilo.

“Nimewasimamisha kazi wauguzi wote waliokuwa zamu jana (juzi) asubuhi, nakuagiza Msajili wa Baraza la Wauguzi uwasimamishe hadi utakapowasafisha kupitia kamati ya msajili,” alisema Dk Kigwangalla.

Mmoja wa wajawazito, Loshan Seif alisema alipowasili juzi asubuhi kwa ajili ya kujifungua, muuguzi mmoja wa zamu alimtaka kulipia Sh5,000 za gloves.

“Siku zote huwa natumia bima lakini jana (juzi) wakaniambia hawatumii, nitoe Sh5,000 za gloves, baadaye niliambiwa natakiwa kuwa na uzi wa mshono, sindano na vingine hivyo kama sina nitoe fedha,” Seif.

Dk Kigwangalla alifanya ziara ya ghafla hospitalini hapo jana saa 9.00 alasiri.

Akizungumza jana alasiri baada ya kufanya ziara ya ghafla Hospitalini hapo na kupata malalamiko hayo kutoka kwa wanawake waliojifungua.

“Mama anaambiwa atoe fedha ya gloves Sh5,000 wakati dukani zinauzwa Sh1,000, nataka liwe fundisho kwa wote wanaotuongezea vifo vya wajawazito kwa tamaa ndogondogo,” alisema Kigwangalla.

Katika ziara hiyo, Dk Kigwangalla alishuhudia ubovu wa vyumba viwili vya upasuaji na kutoa maelekezo kwamba, virekebishwe ndani ya miezi sita.

“Hali ni mbaya ndani ya hizi ‘theater’ zote mbili zifanyiwe ukarabati iwapo itashindikana nitazifunga, lazima ziwe na hadhi yake na nitakuja kukagua,” alisema.

#YALIYOJIRI>>>Polisi Wafanya Upekuzi Nyumbani Kwa Halima Mdee.Fahamu zaidi hapa.

Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam jana lilifanya upekuzi mkubwa katika nyumba ya Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) baada ya kumtilia shaka kuwa na nyaraka muhimu za vikao vya uchaguzi wa Meya wa Jiji hilo.

Kikosi cha jeshi hilo kilifika katika nyumba ya mbunge huyo majira ya saa tisa alasiri na kufanya mazungumzo na Mwanasheria wake, John Mallya ambapo baada ya kukamilisha taratibu za kisheria walianza zoezi la upekuzi uliochukua zaidi ya saa moja.

Kiongozi wa kikosi hicho cha Polisi, aliwaambia waandishi wa habari kuwa walilazimika kufanya upekuzi katika nyumba hiyo baada ya kusadikika kuwa wakati wa vurugu zilizotokea katika ukumbi wa Karimjee jijini humo wikendi iliyopita kufuatia kuahirishwa kwa uchaguzi wa Meya wa Jiji, Mdee aliondoka na faili muhimu lenye madokezo yanayohusu uchaguzi huo.

Hata hivyo, baada ya kukamilisha upekuzi huo, Polisi walijiridhisha kuwa hakukuwa na nyaraka hizo ndani ya nyumba hiyo wala kitu chochote ambacho wangekitilia shaka licha ya kukuta nyaraka nyingi za mbunge huyo. Hivyo, walitoa cheti maalum cha kuthibitisha kuwa hakuwa na nyaraka zozote kinyume cha sheria.

“Wamekagua nyaraka zote. Madai yao ni kuwa Halima alimpora au alichukua nyaraka za kiongozi wa Jiji, lakini wamekuta hakuna jambo lolote ambalo linatiliwa shaka. Na wametoa Certificate inayoonesha kwamba hakuna chochote ambacho kimechukuliwa,” alisema Mwanasheria wa Mbunge huyo, John Mallya.

Mdee alishikiliwa na Polisi na kulala rumande juzi kutokana na tuhuma za kushiriki katika vurugu zilizotokea katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam, Jumamosi, Februari 27.

Wengine wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi ni Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara.

#YALIYOJIRI>>EWURA yatangaza kushuka kwa bei ya mafuta.Fahamu zaidi hapa.

Mkurugenzi wa Mamlaka ya Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Felix Ngamlagosi amesema ‘kuanzia tarehe 2 Machi bei za mafuta zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la Februari 2016.

Kwa Machi 2016 bei ya rejareja za petroli imepungua Tsh 31 kwa lita sawa na 1.70%, Diesel imepungua Tsh 114 kwa lita sawa na 7.10% na mafuta ya taa yamepungua kwa Tsh 234 kwa lita sawa na 13.75%’

‘kwa kiasi kikubwa, kupungua huku kwa bei za mafuta kwenye soko la ndani kumetokana na kuendelea kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia

Habari Katika Magazeti ya Leo siku ya Jumatano ya March 2 yako hapa.


#YALIYOJIRI>>>Serikali Yalitaka Gazeti la DIRA Limuombe Radhi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.Fahamu zaidi hapa.

1. Utangulizi:

Gazeti la Dira ya Mtanzania, Toleo Na.404 la Februari, 29 - Machi 6, 2016 liliandika taarifa yenye kichwa cha habari kisemacho "Uchafu wa Ombeni Sefue Ikulu".  Taarifa hiyo, ambayo ni muendelezo wa makala nyingine kwenye toleo la gazeti hilo la wiki iliyopita, ilimtuhumu Katibu Mkuu Kiongozi kushawishi juu ya uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD pamoja na Kampuni za "CRJE" na "UGG" kupewa tenda ya kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma, Daraja la Kigamboni na Reli ya Dar es Salaam - Kigali. Taarifa zote hizi ni za uongo na za kupotosha wananchi.

2. Kuhusu uteuzi wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa MSD,

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue, hakuhusika kwa namna yoyote kushawishi uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa MSD.

Uteuzi huo ulitekelezwa kwa kufuata kanuni na taratibu zilizowekwa. Nafasi hiyo ilitangazwa na Bodi tarehe 20 Novemba, 2013.

Usaili ulifanywa na kampuni huru iliyopewa jukumu hilo na Bodi. Mapendekezo ya majina matatu yalipelekwa kwa Mhe. Rais na Waziri wa Afya, kwa ajili ya uteuzi.

Balozi Sefue alikuwa hamjui aliyeteuliwa na wala hakuwahi kuwa na uhusiano naye. Alichofanya Balozi Sefue ni kutangaza tu uteuzi baada ya Rais kuteua.

Gazeti hilo pia limeandika uwongo kuwa MSD haijawahi kuongozwa na Mkurugenzi Mkuu asiye Mfamasia.

Tangu MSD ianzishwe mwaka 1993 hadi sasa, ni Mkurugenzi Mkuu mmoja tu, Rino Meyers (1996-1999), ndiye alikuwa Mfamasia. Wakurugenzi wengine kama Peter Mellon (1993-1995), Jay Drosin (2001-2004) na Joseph Mgaya (2004-2013) hawakuwa Wafamasia.

3. Kuhusu Kampuni ya CRJE kuhusishwa na Balozi Ombeni Y. Sefue

Suala la kumhusisha Katibu Mkuu Kiongozi na kampuni hii nalo ni uzushi na uongo wa kupindukia.

Wakati kampuni hii ikipewa tenda ya kujenga Chuo Kikuu cha Dodoma mwezi Oktoba 2007, Balozi Ombeni Y. Sefue hakuwa Katibu Mkuu Kiongozi; alikuwa Balozi wa Tanzania nchini Marekani.

Kadhalika mchakato wa kumpata mkandarasi wa daraja la Kigamboni, ulipoanza mwezi Machi, 2011, Balozi Sefue hakuwa Katibu Mkuu Kiongozi; alikuwa Balozi wa Tanzania, Umoja wa Mataifa, New York.

Hata mkataba wa ujenzi wa Daraja hilo uliposainiwa tarehe 9 Januari, 2012, Balozi Sefue alikuwa na wiki moja tu ya kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kufuatia kuteuliwa tarehe 30 Disemba, 2011.

Aidha, Kampuni iliyoshinda tenda hiyo wala siyo CRJE kama ilivyoandikwa na gazeti hilo bali ni China Major Bridges Engineering Company (BCEC) kwa kushirikiana na Kampuni ya China Railway Construction (CRCEG).

4. Kuhusu tuhuma kuwa Katibu Mkuu Kiongozi kuipigia Chapuo Kampuni ya UGG:

Katibu Mkuu Kiongozi hajawahi kuipigia chapuo kampuni yoyote ile pahala popote. Isitoshe, hakuna kampuni yenye jina la "UGG" iliyowahi kuonesha nia ya kujenga reli ya kati.

Hii ni moja ya uthibitisho kwamba gazeti hili linatoa taarifa za kuokoteza zisizo na ukweli kama vile walivyopotosha kuhusu jina la Katibu Mkuu Kiongozi kwenye makala yao ya pili kwenye ukurasa wa tisa wa gazeti hilo yenye kichwa cha habari "Magufuli anaishi na jipu Ikulu" ambapo walimpachika Katibu Mkuu Kiongozi jina la Sifuni, jina ambalo hajawahi kuwa nalo.

Balozi Sefue hajahusika, hahusiki na wala hatahusika katika kuchagua wa kupewa tenda hiyo kwa sababu yeye si sehemu ya wenye mamlaka ya kutoa tenda.

5. Kuhusu Eliachim Maswi:

Gazeti la Dira ya Mtanzania limeandika kuwa moja ya "madudu" aliyofanya Balozi Sefue ni walichoita kumsafisha Bwana Eliachim Maswi.

Wanadai hivyo wakati wamekiri kuwa alichofanya Balozi Sefue ni kusoma matokeo ya uchunguzi, ambao hakuufanya yeye.

Waliomsafisha Maswi ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali; Sekretarieti ya Maadili ya Umma; na hatimaye kamati ya uchunguzi iliyoongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu. Kwa hiyo, kwa maoni ya gazeti hili, Balozi Sefue asingepaswa kusoma matokeo ya uchunguzi
uliofanywa  na  vyombo  hivyo  huru.     Kwa  maoni  yao  kusoma  taarifa  ya
uchunguzi ni "madudu".

6. Hitimisho:

Kwa kuwa habari hizo hazina chembe yoyote ya ukweli, na wao wenyewe ndani ya gazeti wamekiri hawana ushahidi, ni wazi kuwa habari hizo ni za kubuni na zimetungwa.

Kwa sababu hiyo, Serikali inalitaka Gazeti  la  Dira ya Mtanzania  kukanusha uongo na uzushi wao na kumuomba radhi Balozi Ombeni Sefue, kuiomba radhi Serikali na kuwaomba radhi wote walioumizwa na uzushi huo kwa uzito ule ule uliotumika kuchapisha taarifa hiyo.

Vinginevyo iwapo gazeti la Dira ya Mtanzania lina ushahidi wa huo "uchafu" wa Katibu Mkuu Kiongozi, waupeleke mara moja kwenye vyombo vinavyohusika ikiwamo Sekretarieti ya Maadili na TAKUKURU.

Vinginevyo, hatua zikichukuliwa dhidi yao wasiseme Serikali inavibana vyombo vya habari.

Aidha Serikali inashauri wenye vyombo vya habari, wachapishaji, wahariri na waandishi wa habari wajikite kwenye weledi na ukweli, wafanye utafiti na kuandika mambo waliyo na uhakika nayo, na kamwe wasikubali kutumiwa kuendeleza agenda za watu wengine.

Imetolewa na Idara ya Habari - MAELEZO.
01 Machi, 2016

#YALIYOJIRI>>>>DK. KIGWANGALLA AAGIZA KUFUNGWA CHUMBA CHA UPASUAJI CHA HOSPITALI YA SANITAS YA MIKOCHENI.FAHAMU ZAIDI HAPA.

Naibu wa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameagiza kufungwa mara moja Chumba cha upasuaji cha hospitali ya Sanitas ya Mikocheni Jijini Dar es Salaam baada ya kubaini kuwa na kasoro mbalimbali ikiwemo mfumo na ramani yake kimefungwa kwa kutokidhi vigezo vya kimataifa vya namna chumba hicho kinavyotakiwa kuwa.

Dk. Kigwangalla ametoa agizo hilo mapema jana Februari 29.2016, alipofanya ziara ya kushtukiza kwenye hospitali hiyo majira ya saa nane na nusu mchana ambapo baada ya kutembelea hospitali nzima na kushuhudia namna ya utolewaji wa huduma, hakuridhishwa na hali aliyokutana nayo kwenye chumba hicho na kutoa maagizo kwa Msajili wa Hospitali Binafsi, Dkt. Pamela Sawa kufunga chumba hicho mpaka uongozi wa hospitali hiyo utakapofanya marekebisho ya mapungufu yaliyopo.

“Chumba cha upasuaji hakiko sawa, siwezi kuvumilia kuacha chumba hiki kiko chini ya kiwango cha kimataifa. Rekebisheni chumba hiki kwa kutumia mfumo wa ramani wa wizara,” alieleza Dkt. Kigwangalla wakati wa kutoa maagizo kwa mmoja wa Ofisa wa Hospitali hiyo.

Aidha uongozi wa hospitali hiyo umepewa siku saba wawe wamewasilisha maelezo ya kutowalipa mishahara kwa kipindi cha miezi minne watumishi wake pamoja na jinsi wanavyoteketeza taka hatarishi za hospitali hiyo.

Katika ziara hiyo Naibu Waziri huyo alipata malalamiko kutoka kwa watumishi hao ambao wamelalamikia kukatwa kwa makato ya mafao pasipo kupelekwa mahali husika kwa zaidi ya miaka mitatu na nusu.

Dkt. Kigwangalla alivitaja viwango vya chumba cha upasuaji kuwa kinatakiwa chumba cha kubadilishia mavazi,kunawa mikono,sehemu ya alama maalum zenye rangi nyekundu, meza ya upasuaji, ukanda wa usafi, chumba cha mapunziko baada ya kutoka kwenye upasuaji na chumba cha kusafishia vifaa vya upasuaji na kuna mashine maalum kwa kuwa kila upasuaji una idadi ya vifaa vinavyotumika.

Aliongeza kuwa viwango hivi vinawekwa ili kuepuka maambukizi.
Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa hospitali hiyo, Bi. Gean Cabral alisema watarekebisha mapungufu yaliyobainika pamoja na kufanya yale yote waliyoagiziwa baada ya tukio hilo.

Download nyimbo ya Ruby inayoitwa "Forever".Hapa hapa.


Download nyimbo ya Dogo Janja inayoitwa "My Life".Hapa hapa.


#YALIYOJIRI>>>>Polisi Yaua Majambazi Watatu,Baada ya Kupekeliwa Walikutwa na Ujumbe wa Kamanda Suleiman Kova.Fahamu zaidi hapa.

Watu watatu wanaosadikiwa kujihusisha na vitendo vya kigaidi na ujambazi wameuawa katika majibizano ya risasi na polisi.

Watu hao walikutwa na karatasi yenye ujumbe kwa aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova ulioandikwa:

“Nasaha kwa Kova, mzee andaa kamati ya mazishi ya vipolisi vyako tukiwamaliza tutakufikia wewe.”

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema jana kuwa tukio hilo, lilitokea Jumamosi iliyopita, eneo la Fire, jijini Arusha wakati mtuhumiwa Athumani Kassim alipokamatwa eneo la Engosheraton akiwa na silaha na aliwataja wenzake.

Kamanda Sabas alisema walipopata taarifa kutoka kwa raia wema walio tilia shaka mwenendo wa mtuhumiwa huyo ambaye alipokamatwa, alikutwa na milipuko, makoti makubwa mawili na kofia ya kuficha uso.

“Baada ya mahojiano, alituambia kuna wenzake wawili anashirikiana nao kufanya uhalifu na tuliweka mtego.

“Saa 5 usiku, askari wetu wakiwa wameambatana na Kassim, walipofika jirani kabisa na nyumba hiyo eneo la Fire, alitoa ishara na wenzake wakaanza kuwashambulia polisi kwa risasi,” alidai kamanda huyo.

Hata hivyo, Sabas alisema polisi waliwazidi nguvu na kuwajeruhi wawili kati yao.

Hata hivyo, magaidi hao walimpiga mwenzao risasi na wao walifariki dunia walipokuwa wakipelekwa hospitali.

Alisema kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi, walikuta vitu mbalimbali ikiwamo sare tano za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), kofia tano za kuficha nyuso, vazi moja la karate, pikipiki moja iliyobomolewa na imebandikwa namba bandia.

Alivitaja vitu vingine kuwa ni bendera mbili nyeusi zenye maandishi ya Kiarabu zinazotumiwa na makundi ya kigaidi.

Vitu vingine ni kisanduku cha chuma na hati ya kusafiria ya Abrahaman Athuman Kangaa, iliyotolewa Aprili 2, 2013, simu tano za mkononi na kati ya hizo, moja ilitambulika kuwa ni ya marehemu Mary Joseph aliyefariki kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana Februari 20, mwaka huu, eneo la Engosheratoni pamoja na kifurushi cha unga wa baruti na jambia moja.

Miili ya majambazi hao imehifadhiwa katika hospitali ya Mkoa ya Mount Meru kwa ajili ya utambuzi.