Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. John Pombe Magufuli
akiagana na Rais wa Rwanda Paul Kagame mara baada ya kumaliza mazungumzo yaliyofanyika
Ngurdoto nje kidogo ya jiji la Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya
mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Kenya Mheshimiwa Uhuru Kenyatta, kando
ya Mkutano Mkuu wa 17 wa kawaida wa wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki unaofanyika Mkoani Arusha, ambapo viongozi hao
wamekubaliana kuimarisha mahusiano hususani katika masuala ya kiuchumi.
Baadhi
ya maeneo waliyokubaliana kutilia mkazo katika mahusiano hayo, ni
pamoja na kutekeleza miradi ya maendeleo inayounganisha nchi mbili
ikiwemo ujenzi wa miundombinu, kukuza biashara na kuzalisha ajira
kupitia viwanda.Rais
Uhuru Kenyatta amesema amefurahishwa sana kuona Rais Magufuli yupo
tayari kuhakikisha nchi ya Kenya na Tanzania zinakuwa karibu, na miradi
ya maendeleo inaharakishwa.
"Kwa
sababu nia yetu sisi ni kuona maendeleo ambayo yatagusa mwananchi wa
kawaida, tumalize umasikini, uchumi ukue, na hivyo hatuwezi kufanya
tukiwa tumetengana" Amesisitiza Rais Kenyatta.
Kwa
upande wake Rais John Pombe Magufuli, amesema Tanzania na Kenya zina
kila sababu ya kuimarisha mahusiano ya kibiashara hasa katika ujenzi wa
viwanda utakaozalisha ajira kwa kuwa watu wake ni wamoja.
"Wazee
wetu Mzee Kenyatta na Mzee Nyerere walijenga mazingira mazuri ya kuwa
na nchi hizi mbili wakati wakipigania uhuru, sasa sisi vijana wao ni
wakati wetu kwenda mbele kwa ajili ya maendeleo" amebainisha Rais Magufuli.Dkt.
Magufuli amebainisha kuwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
zinajenga mahusiano na ushirikiano zinalenga kupata manufaa hayo ya
kiuchumi kwa manufaa ya wananchi wake.
Ameutaja
mradi mmojawapo kuwa ni ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka
Tanzania kwenda nchini Kenya kupitia Namanga, na akaongeza kuwa Tanzania
itakapoongeza uzalishaji wa umeme na kuanza kuvuna gesi, itaiuzia pia
Kenya, halikadhalika Kenya nayo itauza bidhaa zake Tanzania.
Kabla
ya kukutana na Rais Kenyatta, Rais Magufuli amekutana na kufanya
mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Rwanda Mheshimiwa Paul Kagame, ambapo
viongozi hao wamekubaliana kuzidisha mahusiano kati ya Tanzania na
Rwanda ambapo Rais Magufuli amemhakikishia kuwa serikali yake
itakamilisha ujenzi wa Reli ya kati kwa kiwango cha kisasa yaani
"Standard Gauge" ili kurahisha usafirishaji wa bidhaa na watu.
Rais
Kagame amempongeza Rais Magufuli kwa uongozi wake bora uliolenga
kuimarisha uchumi, ikiwemo kuimarisha bandari ya Dar es salaam ambayo
Rwanda inaitegemea na ujenzi wa Reli ya Kati ambayo pia ni tegemeo kubwa
kwa uchumi wa Rwanda.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiano, IKULU
Arusha
02 Machi, 2016
0 comments:
Post a Comment