Friday, 22 January 2016

#YALIYOJIRI>>>Gazeti la Jamhuri lapewa siku 7 kukanusha habari waliyoandika kuhusu familia ya Rais mstaafu Kikwete kuhusika katika umiliki wa kampuni ya UDA. -Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Simon Group na UDA, Robert Kisena amesema wasipofanya hivyo watapelekwa mahakamani ili wakatoe ushaidi wa maandishi.Fahamu zaidi hapa.

Gazeti hili kuna tetesi limepewa siku saba kukanusha habari walizochapisha kuhusu familia ya Jakaya Kikwete.
Kama ndivyo, ni muda wa kuona makali ya Nape endapo watakaidi agizo.
Sintoshangaa gazeti la Jamuhuri nalo kupewa hukumu ya kifo.

Gazeti la Jamhuri lapewa siku saba kukanusha habari iliyoandikwa kwenye gazeti hilo Januari 18, 2016 toleo no. 25 lililokuwa na kichwa cha habari FAMILIA YA JK YAHUSIKA UDA habari iliyokuwa ukurasa wa mbele wa gazeti hilo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni ya Simos Group na UDA, Robart Kisena wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo,amesekuwa hakuna uhusiano wa umiliki na familia ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne,Dk Jakaya Kikwete.

Kisena amesema kuwa Familia ya Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne ,Dk. Jakaya Mrisho Kikwete hahusiki kabisa kwani kampuni ya UDA na kampuni ya Simon Kisena haihusiani na familia ya JK hata miradi inayofanywa na Kampuni hiyo.

Aidha amesema gazeti lililoandika habari hiyo linatakiwa kuomba radhi kwa siku hizo kwa kuwa na habari yenye uzito ule ule na ukurasa ule ule.

Kisena amesema wasipofanya hivyo watapelekwa mahakamani ili wakatoe ushaidi wa maandishi mahakamani hapo juu ya uhusikaji wa Familia ya Rais Mstaafu katika kampuni ya usafiri Dar es Salaam (UDA).

Hata hivyo amesema kuwa kampuni ya (UDA) itarudishwa kwa wananchi ifikapo Machi Mwaka huu ili iweze kuendeshwa kwani shirika hili kwa mara ya kwanza lilikua na magari 7 mpaka sasa maari hayo yameongezeka na kufikia zaidi ya magari 400.

0 comments:

Post a Comment