JANA
limetokea tukio la aibu katika nchi yetu pale serikali ilipofanya
jaribio la hatari la kuzuia wananchi kuona na kusikia kinachoendelea
bungeni.
Kitendo
cha serikali ya CCM kuzuia kuonyeshwa moja kwa moja vipindi vya bunge
katika televisheni ya taifa ni cha kijima na sisi chama cha
ACT-Wazalendo tunakilaani kwa nguvu zetu zote.
Tunakitafsiri
kitendo hiki cha serikali kama mwendelezo wa hatua na juhudi za Rais
Magufuli za kuminya demokrasia na kusimika utawala wa kiimla.
Tunawasihi wananchi kusimama imara na kuzipinga jitihada zozote ovu za kuminya demokrasia nchini.
Tunawapongeza
wabunge wazalendo wa upinzani kwa kusimama pamoja na kupinga nia ovu ya
serikali ya kuua demokrasia katika nchi yetu.
Tunawatia shime wabunge wote wazalendo kuendelea kupigania maslahi mapana ya taifa letu.
ACT-Wazalendo! Taifa kwanza leo na kesho!
Imetolewa na;
Samson Mwigamba,
KATIBU MKUU.
0 comments:
Post a Comment