Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa leo amefafanua kauli yake ya kupiga marufuku
mikutano ya vyama vya siasa nchini kuwashukuru wananchi hasa kwa wale
wagombea walioshindwa uchaguzi kwa kusema kuwa mwandishi aliyeripoti
tukio hilo alimnukuu vibaya.
“.......na
tumesema, siasa tumeshazimaliza. Sasa tunataka tufanye kazi za
maendeleo. Hatuhitaji tena watu kuja kutuvuruga. Mikutano ya shukrani
itafanywa na wale tu walioshinda kwenye maeneo yao. Wengine watulie.
“Vyama sasa viache wale tu waliochaguliwa kwenye maeneo yao washukuru, wengine hawa watakuja kuleta maneno ambayo yatatuvuruga. " Waziri Mkuu alinukuliwa akiyasema hayo Wilayani Ruangwa mkoani Lindi
“Vyama sasa viache wale tu waliochaguliwa kwenye maeneo yao washukuru, wengine hawa watakuja kuleta maneno ambayo yatatuvuruga. " Waziri Mkuu alinukuliwa akiyasema hayo Wilayani Ruangwa mkoani Lindi
Akijibu
Swali la Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni Mhe. Freeman
Mbowe leo asubuhi kuhusiana na kauli hiyo, Waziri Mkuu alisema kuwa
serikali inaendeshwa kwa mujibu wa sheria na katiba hivyo inatambua kuwa
katika mfumo wa vyama vingi, vyama vya siasa vinaruhusiwa kufanya
mikutano ila kwa utaratibu maalumu.
Waziri
Majaliwa alisema mwandishi aliyemnukuu kuhusiana na kauli hiyo
hakumtendea haki kwa kuwa aliitoa kauli hiyo akiwa kama mbunge wa
kawaida na si Waziri mkuu na yalikuwa ni makubaliano ya vyama vya siasa
katika jimbo lake na kwamba halikuwa agizo kwa nchi nzima.
Waziri
Mkuu huyo aliongeza kuwa kauli hiyo aliitoa wakati alipokutana na
madiwani na viongozi wengine wa mkoa wake ambapo walikubaliana kuweka
siasa pembeni na kufanya kazi kwa pamoja katika kuleta maendeleo.
0 comments:
Post a Comment