Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema kwamba matangazo ya bunge hayatarushwa
yote live kama serikali ilivyosema jana na tayari hatua hiyo imekwisha
kuanza.
Majaliwa
ameyasema hayo alipokuwa akijibu swali la papo kwa papo la Mbunge wa
Hai ambaye pia ni msemaji wa kambi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe
aliyetaka kujua kwanini serikali imefanya maamuzi ya kuzuia wananchi
wasione matangazo ya Bunge moja kwa moja.
Akijibu
swali hilo Waziri Mkuu amesema kwamba uamuzi wa kutoonyeshwa kwa
matangazo ya moja kwa moja uliombwa na chombo cha umma chenyewe kwamba
hakina uwezo kujiendesha na uamuzi wao huo umeungwa mkono na serikali.
''Maamuzi
ya chombo hiki yameungwa mkono na serikali na waziri Nape Nnauye
amefanya kipindi maalum kuhusiana na jambo hilo na wananchi wameelewa
vizuri na wameiunga mkono serikali kwamba matangazo yatarekodiwa na
yatarushwa kama kipindi maalum usiku'' Amesema Waziri Majaliwa.
0 comments:
Post a Comment