BASI
la kampuni ya Mohammed Trans aina ya scania T.858.AWY lililokuwa
likitokea jijini Mwanza likielekea jijini Dar-es-salaam,juzi lilipata
ajali na kusababisha kifo cha utingo wake na kujeruhi vibaya abiria
wanne.
Utingo huyo aliyefia hospitali ya wilaya ya Iramba akipatiwa matibabu,ni Abdallah Athuman (35) mkazi wa Shinyanga mjini.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake jana, Kaimu kamanda wa jeshi la
polisi mkoani Singida, ACP Simon Haule, alisema ajali hiyo imetokea
Januari 9 mwaka huu saa 6.45 mchana huko katika mlima Sekenke wilaya ya
Iramba.
Alisema
siku ya tukio basi hilo lililokuwa likiendeshwa na Jovin Jonson (35)
lilipofika eneo la tukio,liligonga kingo za daraja na kusababisha kifo
cha utingo na abiria wengine wanne kujeruhiwa.
Haule
alitaja waliojeruhiwa kuwa ni mkazi wa Kahama mkoani Shinyanga Asha
Said (20) mkaguzi wa ndani wa mahesabu wa kampuni ya Mohammed ambaye
amekatika mguu wa kushoto.
“Mkulima
na mkazi wa Tengo wilaya ya Kahama,Lucas Deo (22) amevunjika miguu yote
miwili na wote wawili na mwenzake Asha,wamehamishiwa hospitali ya rufaa
Bungando jijini Mwanza kwa matibabu zaidi”,alisema kaimu kamanda huyo.
Haule
allisema Felix Matimati (30) mkazi wa Shinyanga mjini,yeye ameteguka
mguu wa kushoto na amepatiwa matibabu ya kuruhusiwa,wakati Alafati Said
(24) mkazi wa jijini Mwanza,amepata majeraha mguu wa kushoto,ametibiwa
na kuruhusiwa.
Kaimu
kamanda huyo,alisema chanzo cha ajali hiyo ni hitilafu ya usukani wa
basi hilo na hivyo kupelekea dereva Jovin kushindwa kulimudu.Dereva huyo
hivi sasa anashikiliwa na polisi
0 comments:
Post a Comment