Spika
wa Bunge, Job Ndugai, anatarajia kutangaza kamati za Bunge leo chini ya
utaratibu mpya na kwamba leo atatangaza Kamati ya Kanuni pekee.
Baada
ya kuitangaza kamati hiyo, nyingine zilizobaki atazitangazia mjini
Dodoma wakati vikao vya Bunge vitakapokuwa vikiendelea mwishoni mwa
mwezi huu.
Utaratibu
huo umebainishwa na Ndugai jana alipoulizwa iwapo Kamati za Bunge
zitatangazwa kabla ya kuanza kwa Bunge lijalo Januari 26, Mwaka huu.
“Kesho (Leo) nitatangaza kamati moja tu ya kanuni na nyingine nitazitangazia mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa Bunge lijalo,” alijibu kwa ufupi.
Taarifa
za kuaminika zinasema kwamba Spika Ndugai amepanga kupunguza wingi wa
Kamati za Bunge ili kuendana na uchache wa wizara zilizopo.
Taarifa
zaidi zinasema kuwa sababu kubwa ya kufanya hivyo ni kuhakikisha kamati
zinakuwa chache lakini zilizo na uwezo wa kufanyakazi kwa kasi ambayo
itaisaidia serikali ya awamu ya tano.
Baada
ya leo kutangaza Kamati ya Kanuni, Spika Ndugai atabaki na jukumu la
kutangaza kamati nyingine 14 mjini Dodoma, iwapo hakutakuwa na ongezeko
la kamati.
Kamati
za Bunge huundwa kwa mujibu wa Katiba Ibara ya 96, likiwa limepewa
madaraka ya kuunda kamati za Bunge za aina mbalimbali na muundo wake
umefafanuliwa na Kanuni za Kudumu za Bunge.
Katika
muundo huo zipo kamati za kisekta na zile zisizokuwa za kisekta, ambazo
kwa pamoja hufanyakazi na kutekeleza majukumu yao kwa niaba ya Bunge.
Kwa
mujibu wa Kanuni ya 89 Bunge limeunda Kamati 15, ambapo baadhi ya
kamati hizo ni Kamati ya Haki, Maadili, Kinga na Madaraka ya Bunge na
Kamati ya Uchumi, Viwanda na Biashara.
0 comments:
Post a Comment