Mashindano ya Mapinduzi Cup yashika kasi baada ya URA ya Uganda kuing’oa Yanga katika michuano ya Kombe la Mapinduzi, hapo jana.
Wakati
wengi walitarajia fainali itakuwa Simba dhidi ya Yanga, lakini timu
zote zimeshindwa kufika fainali baada ya Mtibwa Sugar kuing’oa Simba
katika mechi ya jioni na Yanga ikaondolewa na Waganda hao kwenye Uwanja
wa Amaan, Zanzibar.
URA imeitoa Yanga kwa mikwaju 4-3 ya penalti baada ya timu hizo kwenda sare ya 1-1 katika dakika 90.
Yanga
walipata bao kupitia Amissi Tambwe katika dakika ya 13 aliyefunga kwa
kichwa, URA wakasawazisha kupitia David Lwasa katika dakika ya 83 baada
ya kuutegua mtego wa kuotea wa mabeki wa Yanga uliongozwa na Vicent
Bossou.
Wakati
wa mikwaju ya penalti, Geofrey Mwashiuya na Malimi Busungu walikosa
upande wa Yanga wakati Simon Sekito alikosa upande wa URA.
YANGA: Wamepata penalti 3
Kelvin Yondani PATA
Geofrey Mwashiuya KOSA
Malimi Busungu KOSA
Simon Msuva PATA
Deo Munish PATA
URA: Wamepata penalti 4
Jimmy Kulaba PATA
Simon Sekito KOSA
Sidi Kieune PATA
Deo Otieno PATA
Brian Bwete PATA
0 comments:
Post a Comment