Baraza Kuu la Chama Cha Wananchi (CUF), leo linatarajia kutangaza uamuzi mzito kutokana na kikao cha Kamati ya Utendaji, kilichofanyika jana jijini Dar es Salaam chini ya Katibu Mkuu wake, Maalim Seif Sharif Hamad.
Kikao
hicho cha Kamati ya Utendaji kilifanyika kwa saa tatu kujadili suala la
tarehe iliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ya kurudia
uchaguzi wa Zanzibar, uliofutwa Oktoba 28, mwaka jana.
Kamati
hiyo ambayo ilikuwa na ajenda moja pekee, ilijadili na kutoa uamuzi
mzito ambayo yatawasilishwa kwenye Baraza Kuu leo na kutolewa kwa umma.
Mmoja
wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji, ambaye hakutaka kutajwa jina ,
alisema kuwa maazimio yaliyotolewa na kikao hicho kilichoanza saa nne
asubuhi, yataishangaza dunia.
Alisema
uchaguzi uliotangazwa na ZEC kuwa utafanyika Machi 20, mwaka huu, ni
batili kwa kuwa tayari mshindi wa uchaguzi huo anafahamika ni Maalim
Seif.
“Jukumu
kubwa la kikao cha Kamati Tendaji kwa mujibu wa Katiba (ya CUF) ni
kuandaa ajenda kwa ajili ya kikao cha Baraza Kuu litakaloanza kesho
(leo) na baada ya hapo tutatangaza msimamo wetu juu ya uchaguzi huo,” kilieleza chanzo hicho.
Kwa
mujibu wa Ofisa Habari wa CUF, Silas Bwire, Kamati ya Utendaji ilikuwa
na wajumbe 18 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, ambao ni viongozi
waandamizi wa chama.
Baraza kuu ambalo linatarajia kufanya kikao chake leo, litakalopokea ajenda zilizojadiliwa jana, lina wajumbe 60.
Kikao
cha Baraza ambacho kitaongozwa na Mwenyekiti wake, Dk. Twaha Tasilima,
kitajadili kwa kina ajenda zitakazowasilishwa pamoja na kuzitolea
uamuzi.
==>Wakati
hatima ya CUF kushiriki au kutoshiriki uchaguzi wa marudio inatarajia
kufahamika leo, mgawanyiko mkubwa umeibuka miongoni mwa wajumbe wake wa
Baraza Kuu la Uongozi Taifa.
Katika mgawanyiko huo, wamo wanaopinga kushiriki huku wengine wakitaka chama kuangalia upya msimamo wa kususia uchaguzi huo.
==>Akizungumzia
mgawanyiko huo, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa CUF, Ismail Jussa Ladhu,
alisema kutokana na ukubwa na uzito wa mgogoro wa uchaguzi, mgawanyiko
ni jambo ambalo halikwepeki kwa chama kikubwa kama hicho.
Alisema
uongozi wa chama uko makini katika kujadili ajenda ya mgogoro wa
uchaguzi na kuwataka viongozi na wanachama pamoja na wananchi kwa ujumla
kuwa na moyo wa subira wakati Baraza Kuu la Uongozi la Chama
linajiandaa kutoa kauli ya mwisho juu ya hatima ya uchaguzi huo.
Jussa
alisema uamuzi utakaotolewa na Baraza Kuu ndio utakuwa mwongozo kwa
wagombea wote wa chama pamoja na wanachama na watu wanaokiunga mkono
chama.
Alisema
mchezo aliyoufanya Jecha wa kufuta matokeo ya uchaguzi kwa manufaa ya
CCM, haukubaliki katika misingi ya demokrasia na utawala bora.
0 comments:
Post a Comment