Rais
wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Magufuli amesema kuanzaia
sasa hataki kusikia malalamiko ya wananchi juu ya suala la njaa na
ikitokea akasikia vilio hivyo vikiendelea mkuu wa mkoa husika
atachukuliwa hatua ikiwemo ya kufukuzwa kazi.
Mh.
Magufuli ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Arusha ameyasema
hayo alipokuwa njiani kutoka jijini Arusha kwenda wilaya Monduli kwa
ajili ya kufunga mazoezi ya kijeshi ya kuonyesha uwezo wa medani 2016
yaliyofanyika katika Briged ya 303 iliyoko Monduli.
Aidha
Mh rais Dr. Magufuli amesema ni jambo halikubali kuendelea kusikia
malalamiko ya wananchi juu ya mambo yaliyoko ndani ya uwezo na
yanayoweza kutatuliwa na wakuu wa mikoa na ameendelea kuwataka viongozi
na watendaji wa serikaali kutimiza wajibu ukiwemo wa kuwatumikia
wananchi.
Kuhusu
malalamiko ya wananchi juu ya kero ya rushwa mh Rais amewataka wananchi
hao kuwa wapole kwani kero itashughulikiwa na itapata ufumbuzi kwani
zoezi la kutumbua majipu linaendelea na kwamba kinachofanyika sasa ni
kutumbua majipu yaliyoiva ambayo ni sehemu ndogo tu ya majipu yaliyopo.
Mh Rais kesho anatarajiwa kutoa kamisheni kwa askari wanafunzi katika chuo cha mafunzo ya kijeshi cha TMA monduli.
0 comments:
Post a Comment