Katika
kuhakikisha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji linafanya kazi kwa ufanisi
mkubwa katika kupambana na majanga, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga ameliagiza jeshi hilo kumchukulia hatua kali za
kisheria mtu yeyote atakayekaidi kulipisha gari la Zimamoto na Uokoaji
pindi linapokuwa linawahi eneo la tukio ili kuweza kuzima moto na
kuokoa maisha ya watu pamoja na mali zao.
Waziri
Kitwanga ametoa agizo hilo alipokuwa anamaliza ziara yake katika Makao
Makuu ya Jeshi hilo Kanda ya Ilala, Dar es Salaam mara baada ya Mkuu wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kamisha Jenerali, Pius Nyambacha kubainisha
kuwa mojawapo ya changamoto zinazolikumba jeshi hilo ni ukaidi wa
baadhi ya wananchi kutotaka kupisha gari la Zimamoto pindi linapokuwa
katika harakati za kuwahi eneo la tukio.
“Hivi
hamjui hata msafara wa Rais unalazimika kupisha gari la Zimamoto au
wagonjwa? Iweje leo wananchi wasipishe magari hayo? Simamieni sheria
hii” Alisisitiza Mhe. Waziri.
Aidha Mhe. Waziri aliahidi kushughulikia changamoto zote zinazolikabili Jeshi hilo changamoto hizo ni ukosefu wa vifaa, ufinyu wa bajeti pamoja na idadi ndogo ya Askari.
0 comments:
Post a Comment