BARAZA
la Vijana wa Chadema (BAVICHA) kwa kushirikiana na Umoja wa wanafunzi
wa vyuo vikuu Chadema (Chaso) wametoa siku tatu kwa Rais John Magufuli
kufuta agizo la Shirika la utangazaji la Tanzania (TBC) kutokurusha moja
kwa moja mikutano ya Bunge inayoendelea Dodoma.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam, Katibu Mwenezi Taifa
Bavicha Edward Simbeyi amesema, kitendo kilichofanywa na Serikali ni
udikteta na kwamba, inawanyima wananchi kupata haki yao ya msingi.
“Tunajiuliza
maswali mengi, ni vitu gani wanataka kuficha? Hadi wananchi wasivijue?
Wakati Bunge linatakiwa kuwa masaa matano na dakika 45 sasa kwanini
wanataka kurusha ndani ya saa moja? Haya masaa manne yanaenda wapi?
Amehoji Simbeyi."
Amesema
hata Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 katika
ibara yake ya 18 inatoa uhuru wa kila raia kupata au kupewa habari bila
ya mashariti kama haya tunayoletewa leo.
“Wanaiogopa
mijala inayoendelea Bungeni, Serikali yoyote inayoogopa kukosolewa
lazima itakuwa na mapungufu yake, tunachohitaji ni mikutano uoneshwe
live kila mtu ajue kinachoendelea” amesema Simbeyi.
Mbali
na hilo, wameitaka serikali kutotumia ubabe ndani ya Bunge kwa lengo la
kutaka kuwadhalilisha wabunge wa upinzani, pia Jeshi la polisi
lizingatie maadili katika utendaji wao wa kazi na wasikubaliane na kila
wanalotumwa na CCM hata kama linavunja sheria.
Amesema
kitendo cha Jeshi la polisi kujiingiza katika masuala ya kisiasa ni
kujidhalilisha wao wenyewe na ni hali inayoendelea kuwafanya kupoteza
uaminifu wao ndani ya jamii.
0 comments:
Post a Comment