SERIKALI
imesema kama Shirika la Afya Duniani (WHO), litapitisha matumizi ya
dawa mpya ya ugonjwa Ukimwi wataitumia, lakini kwa sasa haiwezi
kuzungumzia tafiti za ugonjwa huo ambazo zipo nyingi.
Kaimu
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Michael John, amesema kwa sasa zipo tafiti nyingi, lakini wao
kama wizara wanasubiri mwongozo kutoka WHO ambao ndiyo unathibitisha
ubora wa dawa na matumizi yake.
“Zipo
tafiti nyingi tunazisikia zinafanyika, lakini hili la Ukimwi ni mapema
mno kulizungumzia ila kinachohitajika ni kusubiri mwongozo wa WHO ambao
ndio wanatuongoza kwenye orodha ya dawa na matumizi yake katika magonjwa
mbalimbali,” alisema John.
Juzi
mashirika mbalimbali ya habari yalitoa taarifa juu ya utafiti mpya wa
dawa ya mseto ya kimiminika ijulikanayo kama PrEP ambayo inatarajiwa
kuleta faraja kwa wenza ambao mmoja anaishi na virusi vya Ukimwi huku
mwingine akiwa hana.
Dawa
hiyo inadaiwa tayari imeanza kutumika kwa baadhi ya mashoga nchini
Uingereza na Marekani ambapo huweza kuondoa hatari ya kuambukizwa hadi
asilimia sifuri.
Pia
itaondoa changamoto iliyokuwapo katika njia namba moja ikiwa pamoja na
kujikinga na virusi vya Ukimwi, yaani kutumia kondomu wakati wa kufanya
tendo la ndoa.
Kutokana
na matumizi ya kondomu wenzi hao walikuwa hawawezi kupata watoto bila
uwezekano wa kuhatarisha afya ya mwenzi ambaye hana VVU.
0 comments:
Post a Comment