Mkurugezni wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga
SERIKALI
kupitia vyombo vyake vya dola, imetangaza kuzitaifisha mali za wote
waliopatikana na hatia ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi na kueleza kuwa
utaratibu huo ndio utakaoendelea kwa watuhumiwa ambao bado kesi zao
hazijamalizika au hazijapelekwa mahakamani.
Tangazo
hilo la serikali limetolewa leo Januari 28, 2016 na Mkurugenzi wa
Mashtaka Nchini, DPP, Bw. Biswalo Mganga, Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai wa Jeshi la Polisi(DCI), Kamishna wa Polisi, Diwani
Athumani na Mkurugenzi wa Upeleelzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na
Rushwa (TAKUKURU), wakati wa mkutano wao wa pamoja na waandishi wa
habari uliofanyika makao makuu ya Polisi jijini Dar es Salaam.
Katika
kuhakikisha kuwa jukumu hilo linatekelezwa, Mkurugenzi wa Upelelezi wa
Makosa ya Jinai amesema, mwaka 2012 idara yake kwa kushirikiana na Ofisi
ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), kwa pamoja walikubaliana kufanya kazi
ya ufuatiliaji wa mali zinazohusiana na uhalifu kama sheria inavyotaka
na kwa upande wa jeshi hilo tayari kitengo chake cha upelelezi wa makosa
ya uhalifu wa kifedha (Money laundering) kiko kazini.
“Katika
kutekeleza mkakatihuo, Jeshi la Polisi limekamilisha upelelezi wa kesi
23 ambazo ziliwasilishwa kwa DPP na kati ha hizo ,kesi tatu (3)
zimetolewa uamuzi na nyingine ishirini ziko katika hatua ya maombi ya
kupata amri ya Mahakama ili ziweze kuzuiwa au kutaifishwa (Restraint or
confiscation).” Alifafanua Kamishna Diwani Athumani
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Upelelezi kutoka TAKUKURU, Bw. Alex Mfungo,
yeye amesema, taasisi yake imeona hakuna maana yoyote kwa mhalifu wa
Ufisadi na uhujumu uchumi ukamfunga gerezani na kisha kumuachia baada ya
kifungo halafu aendelee kutumia mali alizochuma kwa njia za haramu.
“Tumeona njia mbadala ya kudhibiti hali hiyo na kwa mujibu wa sheria ni kumfilisi mhusika hata kama atatumikia kifungo.” Alibainisha Bw. Alex
Naye
Mkurugenzi wa Mashtaka, DPP, Bw. Biswalo Mganga, yeye amesema ili
kuendana na dhana ya Hapa Kazi Tu, ni lazima kukabiliana na wahujumu
uchumi na Mafisadi ili hatimaye Wananchi walio wengi waweze kunufaika na
rasilimali zao.
“Natoa
wito kwa nyie waandishi wa habari muujulishe umma wa Watanzania kuwa
kama mtu anayo taarifa au anajua mali zinazomilikiwa na mtu isivyo
halali hususan watumishi wa umma basi atoe taarifa.” Alisema
DCI Kamishna wa Polisi Diwani Athumani
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, TAKUKURU, Bw. Alex Mfungo
DCI Kamishna wa Polisi Diwani Athumani
Bw. Mfungo, (kulia), akiwa na DPP, Mganga.
0 comments:
Post a Comment