Timu ya Mtibwa Sugar jana jioni imeonyesha ubabe mbele ya Timu ya Simba baada ya kupata ushindi wa goli moja kwa bila baada ya Kiungo
nyota wa Timu ya Mtibwa Sugar, Ibrahim Jeba kuifungia Timu yake ya Mtibwa Sugar na kuiwezesha
timu hiyo kutinga fainali ya Kombe la Mapinduzi na kuivua ubingwa
Simba.
Jeba
ameiwezesha Mtibwa Sugar kutinga fainali kwa bao pekee alilofunga katika
kipindi cha kwanza na kuipa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba.
Jeba alifunga bao pekee katika dakika ya 45 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na Peter Manyika baada ya shuti la Shiza Kichuya.
Hata
hivyo, juhudi za Simba kusawazisha hazikuwa na mafanikio na kikosi hicho
kilionekana kutokuwa na mipango kinapofika langoni mwa Mtibwa.
Mara
mbili, Ibrahim Ajib na Abdi Banda walipiga mashuti yaliyookolewa na kipa
Said Mohammed Nduda na kufanya matokeo yabaki yalivyo.
0 comments:
Post a Comment